;
WERNER AKUBALI KUSAINI CHELSEA, MANCHESTER UNITED NA LIVERPOOL KWA VIGEZO - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 30 June 2020

WERNER AKUBALI KUSAINI CHELSEA, MANCHESTER UNITED NA LIVERPOOL KWA VIGEZO

WERNER AKUBALI KUSAINI CHELSEA, MANCHESTER UNITED NA LIVERPOOL KWA VIGEZO
TIMO Werner nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya RB Leipzig inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga amesema kuwa anaweza kusaini kwenye timu zote tatu ambazo zinahitaji saini yake kwa sasa iwapo mojawapo kati ya hizo itatimiza masharti yake.

Miongoni mwa timu ambazo zinampigia hesabu nyota huyo ni pamoja na Chelsea ambayo inapewa nafasi kubwa ya kupata saini ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 24.

Mbali na Chelsea pia Inter Milan, Manchester United na Liverpool nazo pia zimeonyesha nia ya kupata saini ya  nyota huyo  ambaye anapenda kwenda kucheza ndani ya Ligi Kuu England.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa fedha kwake sio jambo la msingi ila anachotazama ni malengo ya timu kufika mbali na kutwaa mataji.

" Fedha kwangu sio sababu ya mimi kwenda kucheza ama kusaini ingekuwa hivyo ningependa kucheza China, ila kwa kuwa Liverpool, Chelsea na United zinanitaka sawa ninaweza kusaini kwa timu ambayo itakuwa bora kwangu," amesema.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB