;
Vanessa Afunguka Kununua Koti la Bil. 4 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 7 June 2020

Vanessa Afunguka Kununua Koti la Bil. 4

Vanessa Afunguka Kununua Koti la Bil. 4
Vanessa Afunguka Kununua Koti la Bil. 4

DAR: Mambo ya fedha! Siku kadhaa zimepita tangu malkia mwingine wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ aposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa amevaa koti analodaiwa kulinunua kwa shilingi bilioni nne za Kibongo na kuzua gumzo kama lote.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

Kama hiyo haitoshi, kuna waliokwenda mbele zaidi na kudai kuwa, koti hilo lilikuwa la mwanamuziki mkubwa duniani, Janet Jackson.

Ikasemekana kwamba, Janet alilivaa koti hilo kwenye ziara yake ya kimuziki iliyokwenda kwa jina la Rhythm World Tour ya mwaka 1990.

Kwa mujibu wa Vanessa na mpenzi wake, Olurotimi Akinosho ‘Rotimi’, koti hilo walilinunua kwa Dola za Kimarekani milioni mbili (zaidi ya shilingi bilioni 4.6 za Kibongo).

Jambo hilo liliwafanya mashabiki wa mwanadada huyo kila mmoja kuongea lake huku baadhi yao wakisema kuwa siyo kweli na hawezi kununua koti kwa kiasi chote hicho cha pesa.

“Vanessa ndiye amefikia levo hizi? Yaani hako kakoti kakinunua bilioni 4.6 za Kitanzania? Mmmh kweli mwaka huu tutaona mengi,” aliandika mmoja wa mashabiki wake kwenye mtandao.

“Bilioni 4 kwa mtoto mzuri kama huyu siyo ishu, halafu watu wanajisahaulisha kweli, Vanessa ni mtoto wa kishua, lakini mbali na yote tunafahamu kuwa amekuwa akijituma sana kufanya kazi.

" Amekuwa akipiga shoo kubwa ndani na nje ya nchi. Mbali na kufanya kazi kwa bidii, lakini hivi karibuni ameangukia kwenye penzi la staa anayefanya poa Marekani.

“Kwa hiyo ni vigumu sana kwa wao kushindwa kununua kwa sababu pia hilo koti ni limited edition, yaani mfano zikitoka kumi katika toleo lake, ndiyo hizohizo hazitoki tena,” alichangia shabiki mwingine.

“Bora hiyo pesa angenunua barakoa ili kusaidia watu wenye hali ya chini kuliko kununua koti la bilioni nne,” alisema shabiki mwingine aliyechangia kuhusu Vanessa kununua koti hilo.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

VANESSA AFUNGUKA

Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Vanessa kwa njia ya WhatsApp ambapo hakuwa tayari kuzungumzia kiundani zaidi, badala yake alisema kwa kifupi tu kuwa, ni kweli amenunua, lakini kwa sasa aachwe atalizungumzia hilo atakapokuwa tayari.

“Mpaka nimeweka kwenye akaunti yangu, ina maana ni ni kweli. Lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote kuhusu hilo kwa sababu siko tayari. Kuna mambo ninayaweka sawa kisha baada ya hapo ndiyo nitakuja kuzungumza,” alisema Vanessa ambaye kwa sasa yupo kwa mchumba wake huyo nchini Marekani.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB