;
Uzee Wampa Mawazo WEMA Sepetu - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 29 June 2020

Uzee Wampa Mawazo WEMA SepetuSTAA asiyechuja miaka nenda rudi, Wema Sepetu amefunguka kuwa hakuna kitu anachokiwazia kwenye maisha yake kama maisha ya uzee na ndiyo maana ameona aanze kujiandaa mapema.

Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni, Wema alisema huko nyuma alikuwa akidhani kuwa maisha hayasogei na umri hauendi, lakini ukweli ni kwamba, kila kitu kinaenda mbele na amegundua hata yeye atapita, watakuja mastaa wengine.


“Sitaki kuwaficha, uzee unaninyima usingizi sana, kuna wakati nawaza kabisa nikiwa mzee nitakuwaje mimi, najua wazi siku si nyingi watatokea Wema wengine, hivyo nimeona ni vizuri kuacha alama nzuri kwa mashabiki zangu na watu wengine maana kuna umri ukifika, vitu vyote unaviacha,” alisema Wema.

Stori:Imelda Mtema


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB