;
Serikali Yataifisha Dhahabu ya zaidi ya Tsh. Billion 2.9 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 28 June 2020

Serikali Yataifisha Dhahabu ya zaidi ya Tsh. Billion 2.9Serikali imetaifisha dhahabu ya Kilogram 27.488 yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.9 iliyoingizwa kinyemela kutoka Kenya
-
Dhahabu hiyo mali ya Mfanyabiashara Bhawesh Chandulal Gandecha, ilikamatwa na Afisa Forodha katika mpaka wa Tanzania na Kenya huko Sirari, Mei 15, 2020
-
Meneja wa TRA Mkoa wa Mara, Wallace Mkande, amesema Mfanyabiashara huyo alikamatwa akitaka kuingiza dhahabu hiyo kutoka Kenya kinyemela bila kuwa na nyaraka za kuonesha amelipia ushuru
-
Mfanyabiashara huyo alipoulizwa alisema ameshalipa ushuru ila hajapewa stakabadhi na kuwa nyaraka nyingine zipo Dodoma huku akipiga simu kwa baadhi ya watu kuwalalamika kwa kushelewesha kuzituma
-
Alifunguliwa kesi Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kushtakiwa kwa makosa ya Kuendesha Mtandao wa Uhalifu, Kufanya biashara ya dhahabu bila nyaraka muhimu na kutakatisha fedha

#JamiiForums - #regrannPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB