;
RASMI: FRAGA AFUNGUKA HAYA KUHUSU SIMBA S.C..!! - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 29 June 2020

RASMI: FRAGA AFUNGUKA HAYA KUHUSU SIMBA S.C..!!

RASMI: FRAGA AFUNGUKA HAYA KUHUSU SIMBA S.C..!!

KIUNGO wa  Simba raia wa Brazil, Gerson Fraga, amesema anapopewa nafasi ya kucheza anajitoa na kujituma kwa lengo la kuisaidia timu yake kupata matokeo mazuri Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.

Fraga aliyesajiliwa na Simba msimu huu, amekuwa akionesha kiwango cha juu anapoanzisha katika kikosi cha kwanza cha Wekundu wa Msimbazi. Akizungumza na tovuti ya klabu  ya simba, Fraga, alisema atafanya vizuri kila dakika atakayopewa kuingia uwanjani kucheza.

Fraga alisema anafanya hivyo ili kuendelea kuwapa raha mashabiki ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kila mechi na kuwasapoti. “Mimi kama mchezaji kazi yangu ni kuhakikisha naisaidia timu kushinda kila mchezo ambao nitapata nafasi ya kucheza.

“Lengo langu nikuisaidia Simba kutwaa ubingwa na kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika mwakani,” alisema  Fraga. Kiungo huyo amewataka wadau wa Msimbazi, mkuendelea kuisapoti timu popote walipo katika michezo iliyosalia  ili kuwaongezea  hamasa  ya kupigania ushindi.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB