;
Mzee Yusuf ‘Amkataa’ Dada’ke - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 7 June 2020

Mzee Yusuf ‘Amkataa’ Dada’keDAR: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab ambaye alimgeukia Mungu wake na kufikia hatua ya kuwa Alhaj, Mzee Yusuf ambaye ametangaza kurudi mjini, amekataa kumjumuisha dada yake, mwimbaji Khadja Yusuf kwenye safari yake ya kurudi mjini. 

Mzee Yusuf  katika safari yake ya kurudi mjini, kwanza hana sababu ya kulifufua kundi lake la zamani la Jahazi Modern Taarab kwani anatarajia kuja na kitu kipya huku jina la Safina likitajwa. 

Akielezea safari yake ya kurudi mjini alipoulizwa juu kumshirikisha mkewe kwenye kundi hilo alisema ni lazima afanye hivyo. 

“Ule ni ubavu wangu siwezi kuuacha popote niendapo ni lazima niwe naye,” alisema Mzee Yusuf. 

Kuhusu kumshirikisha dada yake, Khadija aliyefanya naye kazi kwenye makundi mbalimbali kama vile Zanzibar Stars Modern Taarab, East African Melody na Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf alisema hana mpango huo. 

“Mpaka sasa bado sina mpango huo kwa kuwa yule ni dada yangu, lakini simmiliki mimi, naweza nikamuambia akanikatalia. 

“Kwa hiyo siwezi kuanza kujitapa kuwa nitakuwa naye halafu akatae, labda apende mwenyewe,” alisema Mzee Yusuf ambaye suala lake la kurejea kwenye Taarab limekuwa na maoni tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki huo.
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB