;
Mastaa Saba Simba Kuiwahi Azam Fc - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 28 June 2020

Mastaa Saba Simba Kuiwahi Azam Fc


MECHI kati ya mabingwa watetezi Simba wakiwa ugenini katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza dhidi ya Tanzania Prison kipindi cha kwanza kimemalizika kwa suluhu kwa maana hakuna timu yoyote iliwezeka kuona lango la mwenzake.

Katika mchezo huo kulikuwa na mashambulizi ya hapa na pale baana ya timu zote mbili kama kile kichwa ambacho alipiga straika wa Tanzania Prison, Jeremia Juma ambacho kama si umahili wa kipa wa Simba Aishi Manula basi walikuwa wanafungwa bao la kuongozwa.

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck ameingia katika mchezo huo akifanya mabadiliko ya wachezaji wa saba ambao wamezoeleka kucheza katika kikosi cha kwanza na pengine amefanya hivyo kutokana na uwepo wa mechi ya nusu robo fainali ya kombe la Shirikisho (ASFC).

Simba watacheza mechi ya robo fainali ya FA, ambayo bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa kwa maana kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Azam na pambano lao litapigwa Jumatano wiki ijayo katika uwanja wa Taifa.

Wachezaji hao saba wa kikosi cha kwanza ambao wamekosekana katika mchezo wa leo ni nahodha John Bocco, Pascal Wawa, Luis Jose, Cletous Chama, Mohammed Hussein, Shomary Kapombe na Francis Kahata.

Kukosekana kwa wachezaji hao saba nafasi zao zimechukuliwa na Haruna Shamte, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Ibrahim Ajibu, Hassan Dilunga, Miraji Athumani na Mzamiru Yassin.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB