;
GOMEZ SASA KUTIMKA NDANI YA MANCHESTER UNITED, DILI LAKE KESHO LINAFIKA MWISHO - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 29 June 2020

GOMEZ SASA KUTIMKA NDANI YA MANCHESTER UNITED, DILI LAKE KESHO LINAFIKA MWISHO

GOMEZ SASA KUTIMKA NDANI YA MANCHESTER UNITED, DILI LAKE KESHO LINAFIKA MWISHO

OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amekubali kuacha kinda wa timu hiyo Angel Gomes kusepa ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo mwenye miaka 19 kesho dili lake ndani ya United linafika tamati na amegoma kuongeza dili jingine kutokana na kutokubali mkataba aliopewa.

Kiungo huyo anatajwa kuibukia ndani ya Chelsea na Juventus ambapo Jumanne atakuwa mchezaji huru baada ya Solskjaer kuthibitisha kuwa kinda huyo hajasaini.

Solskjaer amesema kuwa ana matumaini kinda huyo atakubali kubaki ndani ya klabu hiyo kwani alikuwepo hapo tangu akiwa na miaka sita na ana tuzo ya mchezaji bora aliyoipata 2017 akiwa ni kiungo kwenye timu ya vijana.

 "Jibu ni fupi ni kwamba mpaka sasa sijapata taarifa mpya kuhusu yeye inaonekana hapendi kuwa hapa," amesema.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB