;
Gabo Afunguka Sababu ya Kufunga Ndoa ya Siri - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 30 June 2020

Gabo Afunguka Sababu ya Kufunga Ndoa ya Siri


Kutoka kiwanda cha BongoMovie msanii wa filamu Gabo Zigamba, amefafanua sababu za kufunga ndoa ya siri kwa kusema mambo ya kuoa ni vitu binafsi vya mtu, pia huwa hapendi kuzungumzia jambo hilo.


Taarifa za msanii huyo wa filamu kuoa zilikuja baada kusambaa kwa picha mitandaoni, siku ya Aprili 21, zikimuonesha katika mavazi na mazingira ya harusi yaliyoashiria kwamba anafunga ndoa.

Akizungumzia suala hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, Gabo Zigamba ameeleza kuwa, "Huwa sipendi kuzungumzia hivyo vitu kwa sababu kuna vitu viwili, kwanza mtu anayeniona anatafuta uhamasishaji kutoka kwangu,sasa kuhusu ndoa siwezi kumhimiza mtu na haifanani kabisa sawa na duka la vipodozi kwenda kuulizia sigara".

"Pili Suala la mimi kuoa au kutokuoa kwa mtu ambaye anamfuatilia Gabo Zigamba haimsaidii chochote, kuoa, kuolewa au kufanya maulid  haina uzito wowote kwa jamii, hayo ni mambo ya mtu binafsi japo Ulaya wanafanya sana hizo Style kwa sisi bado hasa ukiangalia soko letu halipo rasmi, kuna vitu vingi vya kupiga kelele ili tuweze kusogea" ameongeza.Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB