;
Diamond Amtajirisha Mbosso - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 7 June 2020

Diamond Amtajirisha Mbosso

Diamond Amtajirisha Mbosso

DAR : Kwa mambo makubwa aliyoyafanya bwa’mdogo kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Yusuph Mbwana Kilungi ‘Mbosso’, ni dhahiri kutamka kwamba, bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiye aliyempa fursa ya kuwa tajiri, Gazeti la IJUMAA lina habari ya kukutia moyo wewe mwenye hasira ya kusaka mafanikio.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

Mbosso ambaye historia yake ya muziki ilianzia Yamoto Band chini ya Mkubwa Fela (Said), amefanikiwa kumiliki mali mbalimbali ambapo kwa ujumla wake inatosha kabisa kumuita bosi.

MALI ZENYEWE

Mbosso ana nyumba ya kisasa ambayo ni ya ghorofa anayoishi mwenyewe jijini Dar es Salaam, lakini kama hiyo haitoshi, anamiliki gari aina ya Toyota Prado ambalo ni moja kati ya magari ya ndoto yake.

WAZAZI WAKE

Kwa upande wa wazazi wake, Mbosso amewanunulia gari aina ya Toyota Alphard ambalo amewapa kwa ajili ya mizunguko ya kifamilia.

Gari hilo wanalitumia kwa mizunguko ya kutoka Kibitimkoani Pwani (kijijini kwao) kwenda jijini Dar kupata mahitaji yao lakini pia, Mbosso amewajengea nyumba wazazi wake hukohuko Kibiti.

Gazeti la IJUMAA linafahamu kwamba, jamaa huyo kwa sasa yupo vizuri licha ya kuwa hana muda mrefu ndani ya WCB chini ya Diamond au Mondi.

“Yupo vizuri, akaunti inasoma vizuri, lakini pia kuwajengea nyumba wazazi, kuwanunulia gari na ukijumlisha na maisha anayoishi yeye hapa mjini ya kifahari si haba, anapaswa kumshukuru Mungu kwa kweli,” alisema mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina.

Mtu huyo alisema, Mbosso ana kila sababu ya kumshukuru Mungu kwani baada ya kundi la Yamoto Band kuvunjika, alipata msoto mkali ambao ulimsababisha aingie kwenye vitendo vya kihalifu.

“Wewe vuta picha mpaka jamaa alifikia hatua ya kukaba na bisibisi, unafikiri kama si Mondi kumchukua sasa hivi angekuwa wapi?” alisema mtu huyo.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

MWENYEWE AFUNGUKA

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA juu ya mafanikio yake, Mbosso alisema kuwa, yeye ni mtu ambaye anaishi katika imani ya dini yake, akiamini kuwa kama Mwenyezi Mungukampangia kupata basi atapata, kila alichokitaka katika maisha yake, alimuomba Mungu.

“Mimi nilikuwa mtu wa ibada sana, nimeswali sana, hata ukiwauliza wenzangu tuliokuwa pamoja Yamoto Band, watakwambia hilo, nakumbuka hata kipindi cha Mfungo wa Ramadhani nilikuwa nakwenda kukutana na watu kwa ajili ya kufanya ibada.

“Naamini nimepewa kipaji cha kutafuta riziki, kwa nini nipishane na kuwa karibu na Mola wangu, niliwahi kumwambia rafiki yangu mmoja hivi, natamani siku moja tupate nyumba ambayo tutakaa kila mtu chumba chake maana tulikuwa tunakaa chumba kimoja tu, kweli Mungu akajaalia tukahamia Tegeta (Dar) nikapata gari pia.

“Nikamwambia pia natamani nimalizie nyumba ya wazazi wangu, natamani wapate gari ya familia, nikimaliza yote hayo natamani kuendesha Prado, nakumbuka kuna kipindi cha Ramadhani ilikuwa usiku nilikwenda kuswali nikiwa na bro wangu Jay Mo, nikaswali na nikaomba Mwenyezi Mungu anitimizie baadhi ya ndoto zangu, anipe hekima na busara kwa viongozi wangu, niwe mwenye kukumbuka nilikotoka, nisiwasahau watu walionisaidia, nisiwe mshamba wa mafanikio, anipe nguvu za kuwasaidia wazazi wangu, yaani huwa namuomba Mungu vitu vingi sana.

MWAKA JANA HAKUFANIKIWA

“Kwa mwaka jana sikufanikiwa kutimiza ndoto zangu, ila kwa mwaka huu namshukuru Mwenyezi Mungu kanijaalia nimeweza kuwakabidhi wazazi nyumba japo kuna vitu hatujamalizia, nimewapa gari ambalo nina imani litawasaidia, maana familia kubwa watoto tuko wengi na wajukuu wengi kidogo, hata wakipata safari yoyote wanatosha kwenye gari,’’ alisema Mbosso, staa wa Ngoma ya Shilingi.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

Mbosso alimalizia kwa kuwaasa vijana kuwa waamini katika kile wanachotaka kukifanya, kukubali kuteseka, kuwa na heshima, kuomba sana kwa Mwenyezi Mungu kwa imani ya dini zao, kuwaombea wazazi na kuwa wanyenyekevu.

TUJIKUMBUSHE

Mbosso alifanya vizuri miaka ya nyuma na nyimbo kadhaa akiwa na Yamoto Band kama vile Mama, Cheza kwa Madoido na Niseme kabla ya kundi hilo kusambaratika.

Baada ya kundi kusambaratika, Mbosso alijiingiza kwenye vikundi vya kihalifu baada ya kuona wenzake kama vile Aslay na Beka Flavour na Enock Bella wanafanya vizuri kwenye gemu huku yeye akishindwa kufurukuta.

Baadaye, Mondi aliamua kumsaidia na kumsaini WCB ambako ndiko kulikompa jeuri na mafanikio makubwa kwenye maisha yake.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB