;
Cristiano Ronaldo, mwanasoka wa kwanza bilionea duniani - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 7 June 2020

Cristiano Ronaldo, mwanasoka wa kwanza bilionea duniani

Cristiano Ronaldo, mwanasoka wa kwanza bilionea duniani
Cristiano Ronaldo, mwanasoka wa kwanza bilionea duniani

Mshambuliaji wa Juventus ya Italia, Cristiano Ronaldo ameweka rekodi nyingine kwa kuwa mwanasoka wa kwanza bilionea duniani.

Kwa App ya Mapenzi; udaku na michezo»»BOFYA HAPA KUPAKUA APP ISIYOTUMIA DATA NYINGI

Mwaka uliopita Ronaldo aliingiza $105 milioni (TZS243.3bilioni) kabla ya kodi na ada nyingine, hivyo kushika nafasi ya nne kati ya mastaa 100 wa Jarida la Forbes.

Kipato hicho kimemfanya Ronaldo kuwa mchezaji soka pekee katika historia kuwahi kupata $1bilioni (TZS2.3trilioni) katika muda wake wa soka.

Nyota huyo mwenye miaka 35 amekuwa mwanamichezo wa tatu kufikia hatua hiyo akiwa bado anacheza baada ya TigerWoods mwaka 2009 na Floyd Mayweather mwaka 2017.

Ronaldo ameingiza jumla ya $650 milioni(TZS1.4 trilioni) ndani ya uwanja katika kipindi cha miaka 17 ya soka la kulipwa, na anatarajiwa kufikia $765 milioni(TZS1.8trilioni) katika mshahara wake kutokana na mkataba wake wa sasa unaoishia Juni 2022.
Mapato ya nyota huyo kwa mwaka 2020 yanajumuisha mshaharawa $60milioni(TZS139 bilioni), kiwango hiki ni kidogo ikilinganishwa na mwaka 2019 kutokana na mchezaji huyo kuridhia kukatwa 30% kutokana na janga la corona.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB