;
BALAMA MAPINDUZI AWASHUKURU WACHEZAJI NA MASHABIKI KWA KUMUOMBEA DUA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 29 June 2020

BALAMA MAPINDUZI AWASHUKURU WACHEZAJI NA MASHABIKI KWA KUMUOMBEA DUA

BALAMA MAPINDUZI AWASHUKURU WACHEZAJI NA MASHABIKI KWA KUMUOMBEA DUA

MAPINDUZI Balama amesema kuwa anajiskia faraja kuona wachezaji wenzake na mashabiki wanamuombea apone.

Mapinduzi aliumia kifunda cha mguu kwenye mazoezi walipokuwa wanajiandaa na mchezo dhidi ya Ndanda FC uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kwenye mchezo huo, Yanga ilishinda mabao 3-2 na kuwafanya wasepe na pointi tatu kibindoni na kujikusanyia jumla ya pointi 60 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 32.

Balama amesema:"Ninashukuru kuona wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wananiombea dua ili nipone, nina amini kwamba nitarejea kwenye ubora."

Balama ametupia mabao matatu ndani ya msimu huu wa 2019/20 na ana pasi moja ya bao kati ya mabao 38 yaliyofungwa na Yanga.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB