;
Azam Waitaja Yanga, kipigo cha Kagera - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 28 June 2020

Azam Waitaja Yanga, kipigo cha Kagera

Azam Waitaja Yanga, kipigo cha Kagera

UONGOZI wa Azam FC kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Zakaria Thabith ‘Zaka za Kazi’ umeeleza kuwa wachezaji wao hawakuwa sawa kisaikolojia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Biashara United ulioisha kwa kipigo cha bao 1-0, baada ya kukumbana na matukio ya kuonewa kwenye mchezo wa awali dhidi ya Yanga.

Dhidi ya Yanga matokeo yalikuwa 0-0, ambapo kulionekana makosa ya wazi kwa waamuzi wa mchezo huo, ambapo Azam walilalamika kutotendewa haki.

"Napenda kuwapongeza wapinzani wetu kwani ni dhahiri leo walikuwa bora na ndiyo maana wameibuka na ushindi, tulijitahidi kucheza vizuri lakini wachezaji wetu walionekana kutokuwa sawa kisaikolojia hasa baada ya kuvunjwa moyo kutokana na matukio ya mchezo wetu uliopita dhidi ya Yanga.

“Kwa kawaida hali kama hii hutokea mara nyingi kwa wachezaji, hivyo nadhani ni muhimu kuendelea kutoa wito kwa waamuzi wetu kuwa wajitahidi kusimamia vizuri sheria ili kusaidia ukuaji wa mpira wetu,” alisema Thabith.Joel ThomasDar es Salaam.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB