EYP MGUU KWA MGUU ELIMU JUU YA VIRUSI VYA CORONA NCHINI | EDUSPORTSTZ -->

Type something and hit enter

OnPakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB
EYP MGUU KWA MGUU ELIMU JUU YA CORONA NCHINI
Empower Youth Prosperity (EYP) ni moja ya mashirika machache yasiyo ya kiserikali yaliyolivalia njunga janga la Corona nchini. 

EYP MGUU KWA MGUU ELIMU JUU YA CORONA NCHINI


Empower Youth Prosperity (EYP) ni moja ya mashirika machache yasiyo ya kiserikali yaliyolivalia njunga janga la Corona nchini.

Empower Youth Prosperity (EYP) imepata ushirikiano wa moja kwa mora juu ya uratibu wa elimu kwa vinaja kupitia wataalamu wa hospitali ya rufaa mkoni Mbeya pamoja na wajumbe wa wizara ya afya kupitia kampeni ya  #MikonoSafiTanzaniaSalama.
Virusi vya corona
Dr Eliah Mwakyusa akitoa elimu juu ya Taaluma ya Afya kwa vijana wa EYP mnamo Tarehe 6 April mwaka huu jijini Mbeya, 

Virusi vya corona
Wajumbe wa wizara ya afya kupitia kampeni ya #MikonoSafiTanzaniaSalama- Mafunzo yakitolewa na Bi Aviola Mnamo Tarehe 08, April 2020
Virusi vya corona
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa na mkuu wa shirika hilo Dr Mwakyusa

Kwa mjibu wa mkuu wa shirika hilo Dr Mwakyusa amesema, wameanza Kutoa elimu ya kiafya juu ya janga la corona mkoani Mbeya.

 Anasema, Mimi pamoja na team yangu ya vijana tumekua tukipita maeneo kadha wa kadha ya mkoa wa Mbeya tukitoa elimu juu ya ugonjwa wa Corona, ikiwa ni pamoja chimbuko au asili ya ugonjwa huo, njia za maambukizi na jinsi ya kuepuka janga hili

CORONA NCHINI TANZANIA
Ndg, Ipyana Mwakyusa akiwa mfano wa mbele akitoa elimu ya kunawa kwa maji na sanitizer 

Ndg, Ipyana Mwakyusa  ameendelea kusema kuwa vijana wake wamejitoa kwa dhati licha ya kuwepo na tishio la ugonjwa huu na uwezeshaji wa shughuli hii kwani vijana hutumia vipato vyao kufikia maeneo mengi ya mkoa wa Mbeya.
Virusi vya corona
Moja ya mabango yenye jumbe Kuhusu Elimu ya kujikinga na Corona

CORONA NCHINI TANZANIA
Msisitizo na mna ya kuepuka misongomano ili kujikinga na Corona

CORONA NCHINI TANZANIA
Wananchi wakipewa elimu zaidi

Uongozi wa shirika hilo unatoa shukrani zao za dhati kwa viongozi wa serikali mkoani Mbeya na Tanzania kwa ujumla kwa namna wanavyopambana na ugonjwa wa Corona, wafanyabiashara pamoja na wadau wanaoshirikiana nao kukamilisha zoezi hili nyeti la elimu juu ya corona.
Virusi vya corona
Takribani wakazi zaidi ya 10,500 mkoani Mbeya wamefikiwa na kupewa elimu namna ya kujikinga na Corona

CORONA NCHINI TANZANIA
Msisitizo juu ya madhara ya Misongamano

CORONA NCHINI TANZANIA
Moja ya njia za maambukizi ya  Corona ni pamoja na tabia ya kusalimiana kwa kushikana mikono
CORONA NCHINI TANZANIA
Team ya EYP ikiwa mtaa kwa mtaa

EYP
mpaka sasa imetoa elimu kwa zaidi ya wakazi 1,0500 mkoani Mbeya na zaidi ya Maelfu ya watanzania kupitia mitandao ya kijamii kama twitter, instagram, facebook na whatsapp. EYP inalenga kupeleka elimu hii katika mikoa yote ya Tanzania.
CORONA NCHINI TANZANIA
Baadhi ya wananchi waliofikiwa mkoani Mbeya
EYP inatoa lai kwa viongozi wa serikali, makampuni binafsi, wafanyabiashara na wadau wa afya kuendelea kuchukua tahadari ya ugonjwa huu wa Corona na kuwezesha shirika hilo kadri watakavyoguswa ili kufanikisha sakata hili.

Changamoto kubwa wanayokabiriana nayo ni usafiri pamoja na vitendea kazi (Vifaa) kwa wawezeshaji.


Awali EYP ilikuwa ikifanya shughuli zake za kuhamasisha vijana na kuwawezesha katika maswala ya ujasiriamali, afya na elimu.

JUA ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA CORONA


Virusi vya Corona (Cov) ni familia ya virusi vinavoysababisha ugonjwa kuanzia mafua ya kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.

 soma zaidi pia>>>>>MAGWIJI AFRIKA WAUNGANA KATIKA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Virusi vya Corona vya COVID-19 ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu. Dalili zake ni pamoja na homa, kikohozi, shida katika kupumua, na katika hali ngumu zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha, nimonia, kukosa pumzi, kushindwa kufanyakazi kwa figo na hata kifo.

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB
 
Blog Meets Brand