ZAMALEK WAIPIGA ESPERANCE 3-1 NA KUBEBA TAJI LA SUPER CUP AFRIKA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 15 February 2020

ZAMALEK WAIPIGA ESPERANCE 3-1 NA KUBEBA TAJI LA SUPER CUP AFRIKA

VIGOGO, Zamalek wametwaa taji la nne la CAF Super Cup baada ya kuichapa Esperance ya Tunisia mabao 3-1 Uwanja wa Thani Ben Jassem Jijini Doha, Qatar jana.
Pongezi kwa Achraf Bencharki aliyefunga mabao mawili jana dakika ya pili na 58 baada ya Yousef Ibrahim “Obama” kuifungia bao la kwanza Zamalek, huku bao pekee la Esperance wanaoshikilia taji la Ligi ya Mabingwa likifungwa na Abdelraouf Benguit dakika ya 54.
Mabingwa wa Kombe la Shirikisho 2019/20 wanatwaa taji la pili mfululizo chini ya kocha Mfaransa, Patrice Carteron ambaye alishinda pia taji hilo mwaka jana akiwa na Raja Casablanca ya Morocco Jijini Doha poa akiipiga Esperance.

Patrice Carteron anakuwa kocha wa kwanza kushinda taji hilo mara mbili mfululizo akiwa na timu mbili tofauti.