Njia za Kuacha Pombe - EDUSPORTSTZ

Latest

Njia za Kuacha Pombe

Njia za Kuacha Pombe
Njia za Kuacha Pombe
Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari mbalimbali kiafya na kisaikolojia.

Pata GB 10 Mtinadao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Wengi baada ya kuathiriwa na pombe hutamani kuacha matumizi ya pombe lakini ni wachache tu ndiyo hufanikiwa katika hili.

MWINGEREZA Matt Haig ambaye ameandika kitabu kilichouzika sana cha ‘Reasons to Stay Alive’ anasema yeye akinywa pombe humletea wasiwasi hofu na uoga anatoa ushauri wa namna ya kufanya ili asinywe pombe.

“Hata kama watu hawakulazimishi kunywa nafsi yako tu inajisuta ni kama vile watu wasiokula nyama halafu umekaa kati yao unakula unajiona kama unawakosea unaweza ukajiondoa hapo,” anasema Haig.

Jinsi ya Kuacha Pombe Tumia Mbinu hizi

1. Epuka watu watakaokushawishi kunywa pombe

Mara nyingi kama wewe unapenda kunywa pombe utakuwa na marafiki wanaokunywa pombe pia.

Ni wazi kuwa marafiki wanaokunywa pombe watakuhimiza kunywa hata kwa kukununulia au hata pengine kukukebehi na kukubeza juu ya uamuzi wako wa kuacha pombe.

Hivyo ikiwa unataka kuacha kunywa pombe ni lazima uepuke marafiki au watu wanaoweza kukushawishi kunywa pombe. Unaweza kutafuta marafiki wengine au watu wengine ambao hawatakatisha lengo lako la kuacha pombe.

Soma pia: Aina 8 za Watu Ambazo ni Sumu za Kuepuka Maishani Mwako.

2. Epuka mazingira yatakayokusababisha kunywa pombe

Ikiwa kuna mazingira yanayoshawishi kunywa pombe basi yaepuke. Inawezekana ni nyumbani kwa rafiki zako, hotelini, baa n.k; ikiwa unataka kuacha kunywa pombe basi huna budi kuepuka mazingira haya ambayo yatakushawishi kunywa pombe. 

Kwa mfano Unaweza kujizoeza kukaa kwenye migahawa au hoteli ambazo hazina pombe ili usije ukajikuta umeshashawishika kuendelea kutumia pombe.

3. Usiweke pombe nyumbani au sehemu unayokaa

Kama unatabia ya kuweka pombe nyumbani, sasa inakupasa kuacha mara moja. Hata kama kuna mtu huwa analeta pombe nyumbani unaweza kumwomba kuwa wewe umekusudia kuacha pombe hivyo asilete pombe nyumbani. Kwa kufanya hivi utapunguza hatari ya kushawishika kuendelea kunywa pombe.

4. Wajulishe watu unaacha pombe

Unapowajulisha watu kuwa unaacha pombe ni rahisi zaidi wao kukusaidia wewe kuacha kunywa pombe. Tafuta watu ambao unahisi wanaweza kukusaidia na kukutia moyo katika mkakati wako huu wa kuacha pombe. Kuwajulisha watu pia kutakuhimiza kuacha kwani utaona aibu kwani umeshawatangazia watu unaacha, hivyo kuendelea ni kujiaibisha wewe mwenyewe.

5. Tatua matatizo ya kihisia na kiakili

Mara nyingi wanywaji wa pombe hasa wale waliopindukia, hunywa kutokana na matatizo ya kihisia au kiakili yanayowakabili. Wengi huwa na majeraha kwenye maswala ya kifamilia au mahusiano, kazi, au hata kiuchumi. 

Unaweza kutafuta suluhisho la matatizo haya kwa kuomba ushauri na msaada wa utatuzi kwa washauri nasaha ili kuepuka kunywa pombe kwa kisingizio cha kupoteza mawazo.

Kumbuka pombe huwa haiondoi matatizo haya bali hukufanya kuyasahau kwa muda tu; ikumbukwe kuwa hata wakati mwingine pombe hukusababishia kuyaongeza zaidi.

6. Tafuta kitu mbadala cha kufanya

Ikiwa kuna muda fulani ambao huwa unautumia kwa ajili ya kunywa pombe, basi yakupasa kubadili matumizi ya muda huo. Unaweza kujipangia shughuli nyingine yenye tija kwenye maisha yako kama vile, mazoezi, utunzaji wa bustani, kusoma vitabu, kutazama filamu, kusikiliza mziki, kutunza mazingira n.k. Kwa kufanya hivi utaweza kubana muda wako unaoutumia kwenda kunywa pombe.

7. Weka malengo tekelevu ya kuacha

Wengi hushindwa kuacha pombe kwa sababu hawana malengo yanayotekelezeka ya kuacha pombe. Kwa mfano unaweza kujiwekea mpango huu:

Nitaanza kuacha kwa kunywa chupa mbili tu kwa wiki.
Kisha nitapunguza na kunywa chupa moja kwa wiki
Na hatimaye nitaacha kabisa kwa wiki
Tarehe fulani (00/00/0000) ni lazima niwe nimeacha kabisa.
Ukijiwekea malengo kama haya na ukahakikisha unafanya juu chini kuyatimiza, hakika utaweza kuacha pombe kabisa.

8. Jipongeze wewe mwenyewe kwa kipindi ulichoweza kuacha pombe

Kujipongeza wewe mwenyewe kunakupa hamasa ya kufanya jitihada zaidi katika mpango wako wa kuacha pombe. Kwa mfano ikiwa umeweza kukaa wiki moja bila kunywa basi jipongeze kwa hatua hii na ujitahidi sasa kukaa mwezi au hata mwaka bila kunywa.

9. Usikae na pesa za ziada

Mara nyingi watu wengi hununua pombe kwa sababu wana pesa mfukoni; wanapokuwa hawana pesa hawalewi kabisa. Jambo hili linaweza kuzuilika kwa kubadili mfumo wako wa kutunza pesa. Unaweza kufanya mambo yafuatayo:

Ikiwa unalipwa pesa kila siku, omba upokee malipo kwa mwezi badala ya kila siku. Ikiwa hili haliwezekani unaweza kumwomba mtu unayemwamini akutunzie pesa zako.
Tunza pesa zako kwenye mifumo ya kutunza pesa kama vile benki na simu za mkononi. Kwa kufanya hivi kutapunguza pesa ulizo nazo mkononi.
Kumbuka njia bora zaidi ni kumwomba mtu unayemwamini akutunzie pesa zako na akukabidhi tu pale unapokuwa na hitaji muhimu. Ikiwa una mwenzi mwaminifu anaweza kukusaidia sana kwa hili.

10. Jikumbushe na kutafakari madhara ya pombe

Unapotafakari madhara ya pombe kama vile matatizo ya kiafya, kisaikolojia, kijamii na hata kiuchumi ni wazi kuwa hili litakuhimiza zaidi kuacha pombe. Tafakari madhara ya pombe na uone kuwa unapokunywa pombe unayapata. Kwa kufanya hivi utajijengea fikra za kujitahidi kuacha pombe ili uepuke madhara hayo.

11. Tafuta usaidizi na ushauri wa kuacha pombe

Zipo taasisi na watu mbalimbali wanaowashauri watu walioathirika kwa matumizi ya pombe. Inawezekana ni asasi ya kiraia, kituo cha ushauri nasaha au hata taasisi au kiongozi wa kidini; hawa wote wanaweza kukushauri na kukutia moyo katika mkakati mzima wa kuacha kunywa pombe.

12. Kula lishe bora

Unywaji mkubwa wa pombe huathiri afya ya mwili kwa kiasi kikubwa. Hivyo ni muhimu ukajitahidi kula lishe bora ili kurudisha afya yako pamoja na kutokutoa nafasi ya kuhitaji kujishibisha kwa pombe badala ya chakula. Ni vigumu mtu kunywa pombe nyingi ikiwa mtu amekula na kunywa vinywaji stahiki kama maji jinsi ipasavyo. Hivyo zingatia lishe bora bila kusahau kunywa maji ya kutosha.

Njia nyinginezo za kuacha pombe ni kama;

1.Nenda kwenye migahawa na si baa.

2.Fanya mazoezi tumia ule muda unaokuwa wazi.

3.Weka wazi kwamba hutumii pombe.

4.Epuka makundi au marafiki wanywaji.

 5.Tafuta starehe katika kinywaji mbadala.

6.Badili sehemu ulizokuwa unaenda kupumzika awali na wajulishe watu wako wa karibu.

Mbali na ukweli kwamba pombe ni sehemu kubwa ama kinywaji kinacho furahiwa katika jamii zetu, utamaduni unabadilika.

Takwimu za hivi karibuni kupitia utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha London unaonyesha theluthi ya vijana wadogo hawanyi pombe kabisa.

Japokuwa vijana wadogo ambao wanasumbuliwa na afya ya akili pia wana.tatizo la unywaji pombe kupita kiasi.

Jennifer Griffin, mtaalamu wa afya ya jamii lakini pia meneja wa taasisi ya huduma ya akili ‘Turn2me’ anasema watu wanatakiwa kujikita katika kufanya mazoezi kama njia mbadala, lakini pia kuyapa kipaumbele mahitaji binafsi ya msingi.

Pombe inahusishwa na wasiwasi lakini pia hali ya kukosa raha funaha na kuwa na woga. Lakini kujichanganya ndiyo namna vijana wadogo hufanya ili kujiunganisha na watu na kutengeneza marafiki. Wasipojichanganya kwa kuhofia kunywa pombe wanaweza wakaanza kujitenga kisha wakaanza kuteseka na upweke.

Uelewa juu ya athari za kiafya unazidi kukua. Kila mmoja akubali. Mtu anaposema hataki kunywa pombe usimlazimishe wala usimwuulize mara mbili.

Pata GB 10 Mtinadao yote BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz