ORODHA YA WAOMBAJI WALIODAHILIWA NA CHUO ZAIDI YA KIMOJA | EDUSPORTSTZ -->

Type something and hit enter

OnPakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Orodha ya waliodahiliwa na chuo zaidi ya kimoja.
Mamlaka ya vyuo vikuu nchini imetoa orodha ya majina rasmi ya waombaji waliodahiliwa na chuo zaidi ya kimoja.

Tcu kupitia tovuti yao wameandika yafuatayo:

ORODHA YA WAOMBAJI WALIODAHILIWA NA CHUO ZAIDI
YA KIMOJA KWA MWAKA WA MASOMO 2018/19 


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia umma kuwa imekamilisha 

uhakiki wa sifa za waombaji waliodahiliwa na taasisi za Elimu ya Juu kwa 

mwaka wa masomo 2018/19. Orodha za majina ya waombaji 

zilizowasilishwa Tume na vyuo kwa ajili ya uhakiki zimesharejeshwa vyuoni 

pamoja na matokeo ya uhakiki ili vyuo husika viweze kutangaza majina ya 

waliowadahili. 

Hata hivyo, katika orodha hizo wako waombaji waliodahiliwa na vyuo zaidi 

ya kimoja. Orodha yao na vyuo walivyodahiliwa inapatikana kupitia tovuti ya 

Tume www.tcu.go.tz. Aidha, waombaji wa aina hii wamejulishwa kuhusu 

udahili wao kupitia ujumbe mfupi uliotumwa kwenye namba za simu za 

mikononi walizotumia wakati wa kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo

husika. 

Tume inapenda kuwatangazia wote waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja 

kuthibisha udahili katika chuo kimoja tu mwombaji anachopendelea 

kujiunga. Mwombaji anatakiwa kufuata utaratibu ufuatao:

1) Kunakili namba maalumu (special code) iliyotumwa kwa njia ya 

ujumbe mfupi kwenye simu yake;

2) Kutumia nywila (password) kuingia katika profile yake iliyo katika 

mfumo wa udahili wa chuo anachokipenda kati ya vile alivyodahiliwa;

3) Kuingiza namba hiyo maalumu katika mfumo wa udahili wa chuo ili 

kuthibitisha udahili wake katika chuo hicho; na

4) Kuthibitisha udahili wake katika chuo kimoja kabla ya terehe 5 

Septemba 2018. 

Tume inapenda kusisitiza kuwa, mwombaji atakayeshindwa kuthibitisha 

udahili wake katika muda uliopangwa, atapoteza nafasi yake na kulazimika 

kuomba upya katika awamu zitakazofuata. 

Imetolewa 

na

Katibu Mtendaji 

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

2 komentar

avatar

Jaman samahan..... Kuna waombaji tumechaguliwa chuo zaidi ya kimoja but hatujatumiwa code sijajua utaratibu huu

avatar

Jaman samahan..... Kuna waombaji tumechaguliwa chuo zaidi ya kimoja but hatujatumiwa code sijajua utaratibu huu

Click to comment
 
Blog Meets Brand