Type something and hit enter

On
Ajira za walimu wa shule za msingi  na sekondari zilizotolewa julai mwaka huu  jumla ya Walimu 4,840 waliopangiwa vituo vya kazi kwenye Shule mbalimbali za Msingi na baadhi kwenye Shule za Sekondari nchini.
Ajira za walimu wa shule za msingi  na sekondari zilizotolewa julai mwaka huu

Ajira za walimu wa shule za msingi  na sekondari zilizotolewa julai mwaka huu  jumla ya Walimu 4,840 waliopangiwa vituo vya kazi kwenye Shule mbalimbali za Msingi na baadhi kwenye Shule za Sekondari nchini.

Ajira za Walimu hizo zilizotolewan zinawataka walimu waliopangiwa vituo vya kazi kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri zilipo shule walizopangiwa na baadaye kuripoti kwenye Shule walizopangiwa. Walimu wote wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 23 Julai, 2018 hadi tarehe 7 Agosti, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo:

(i) Vyeti halisi vya taaluma vya Kidato cha Nne na/au Kidato cha Sita;

(ii) Vyeti halisi vya kitaaluma vya mafunzo ya Ualimu katika ngazihusika; na

(iii) Cheti halisi cha kuzaliwa. Walimu wote waliopangiwa vituo vya kazi wanaelekezwa kuwa:

Vituo vyao vya kazi ni Shule ya Msingi au Sekondarializopangiwa na sio Makao Makuu ya Halmashauri; Anuani ya Simu “TAMISEMI” DODOMA Simu Na.: (026) 2333848, 2321607  2322853, 2322420 Nukushi: (026) 2322116, 2322146  2321013 Barua pepe: ps@tamisemi.go.tz Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Barabara ya Mlezi, S.L.P. 1923, DODOMA.

Mwajiriwa atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kasha akaondoka katika kituo chake cha kazi alichopangiwa Serikali itamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo; na
Hakuna Mwalimu atakayekubaliwa kubadilisha kituo kwa sababu yoyote ile. Kila mwajiriwa mpya anapaswa kuripoti katika kituo chake alichopangiwa na si vinginevyo.

Ajira za walimu wapya zinaambatana na sharti kuwa ambao watashindwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa nafasi zao zitachukuliwa na Walimu wengine 5,220 wenye sifa waliokosa nafasi.

TAARIFA YA SERIKALI KWA AJIRA MPYA 6180 PAMOJA NA VIGEZO HUSIKA BOFYA HAPA
Wakurugenzi wa Halmashauri husika wawapokee Walimu waliopangwa kwenye Halmashauri zao kwa kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya kuripoti kwao.

Taarifa ya kuripoti waajiriwa hao itumwe Ofisi ya Rais- TAMISEMI ifikapo au kabla ya tarehe 10.08.2018 baada ya tarehe ya mwisho ya kuripoti. Majina ya Walimu waliopangiwa vituo yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA YA AJIRA ZA AJIRA
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment