BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 30 July 2018

30 July

TIMU ITAKAYOCHEZA NA SIMBA SC SIKU YA SIMBA DAY

Timu itakayocheza na Simba sc siku ya simba day yawekwa wazi
Timu itakayocheza na simba sc siku ya simba day yawekwa wazi

Zikiwa zimebaki siku chache klabu bingwa vpl simba sc, imekatakiu ya mashabiki wake kwa kuweka bayana timu watakayo minyana nayo siku ya simba day. Kupitia ofisa habari wa timu hiyo ndg Hajimanara ameongea nakuweka wazi kuhusu mchezo huo.Manara ameeleza kuwa hivi sasa ni mapema sana kuitaja timu watakayocheza nayo kwani bado nguvu zao zipo katika maandalizi ya msimu ujao ambapo timu imeweka kambi Uturuki.

Manara amesema kuelekea tarehe 2 mpaka 3 Agosti timu hiyo itawekwa wazi lakini kwa sasa haiwezi kutajwa akieleza kuwa wakati mwafaka haujawadia.

Aidha, Manara amesema Simba inaendelea vema na mazoezi huko Uturuki ambapo kila hali ya mchezaji kiafya ipo salama na hakuna aliye majeruhi kwa wakati huu.

Kikosi hicho kimekuwa kikijifua kimazoezi ndani ya Uwanja na nje kwa maana ya kwenda gym kwa lengo la kuwapa wachezaji nguvu ya kuwapa stamina pindi wanapokuwa mchezoni.

Sunday, 22 July 2018

22 July

"MANCHESTER UNITED HAIWEZI KUMNUNUA BALE" BELLAMY

Mchezaji wa zamani wa Wales, Craig Bellamy amesisitiza kuwa Manchester United haiwezi kulipa mshahara wa Gareth Bale ya Real Madrid.
Manchester united wammezea mate bale 

Mchezaji wa zamani wa Wales, Craig Bellamy amesisitiza kuwa Manchester United haiwezi kulipa mshahara wa Gareth Bale ya Real Madrid.


Bale amekua akisadikika kurudi kwenye Ligi Kuu England, baada ya kufanya vizuri nchini Hispania.

Kwa Real madriad kiuza Cristiano Ronaldo kwa Juventus kwa mkataba wa € 100 millioni, itakua gharama kubwa kwa klabu yoyote kumnunua Bale.

Bellamy, akizungumza na Daily Star, anasema hategemei chochote kutokea

"Aende wapi? Manchester United hawezi kulipa mshahara wake, hakuna mtu anayeweza. Kuna klabu moja tu ambayo inaweza kulipa mshahara wake.

"Huu ndio ulimwengu alio nao wakati huu. Mshahara wake ni mkubwa akitaka  kukwenda mahali pengine.


"Na nina hakika atafanya lakini kwa kweli ila ni mtu ganicatakwenda kumunua?

"Klabu inawezaje na kutumia £ 80m, £ 90m?

"Najua Juventus alifanya kwa Ronaldo lakini lengo la Ronaldo ni tofauti, hiyo ni ulimwengu tofauti wa biashara.

"Lakini Gareth, unawezaje kwenda na kutumia £ 80m, £ 90m, £ 100m kwa mchezaji ambaye huwezi kupata kurudi yoyote?

"Labda kama sehemu ya mkataba wa kubadilishana lakini Gareth hatakuwa sehemu ya mikataba yoyote ya kubadilishana, yeye ni mchezaji mzuri sana kwa hilo.

"Kwa hiyo sioni kuwa ni hoja inayowezekana kwa mtu yeyote kupata mahali popote karibu," alisema.

Saturday, 21 July 2018

21 July

KLABU YA SIMBA YAWAHURUMIA WAKIMATAIFA

klabu ya  Simba sc sa  kupitia kwa kaimu Makamu wake wa Rais, Salim Abdallah ‘Try Again’ imesema kuwa haiwezi kusajili mchezaji yoyote kutoka klabu ya Yanga
Klabu ya simba waihurumia yanga

Klabu ya  Simba sc kupitia kwa kaimu Makamu wake wa Rais, Salim Abdallah ‘Try Again’ imesema kuwa haiwezi kusajili mchezaji yoyote kutoka klabu ya Yanga kwa sasa kwakuwa inafahamu hali ngumu inayoikumba klabu hiyo.

Inafahamika kuwa siku za karibuni kumekuwa na tetesi za klabu Simba kutaka kumsajili mchezaji Kelvin Yondani kutoka kwa mahasimu wao baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliokwisha.

Baada ya tetesi hizo kusambaa ndipo uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kuinusuru klabu hiyo, Abbas Tarimba walipokutana na Yondani na kumalizana naye kwaajili ya kuendelea kucheza msimu ujao.

Timu ya simba sc kupitia makamu wake maarufu kama  , Try Again amesema kuwa Yondani ni mchezaji Tegemeo wa Yanga na endapo klabu Simba ikimsajili manaake wataibomoa klabu hiyo na itakuwa haijengi mpira wa Tanzania akilinganisha na usajili wa msimu uliokwisha wa Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajibu kwa klabu hizo.

“ Tunafahamu Yanga wako kwenye matatizo, na hali ngumu sasa tunapoendelea kuwabomoa hatuusaidii mpira bali tunaudidimiza mpira “. Amesema Salim Abdallah

 Klabu ya Simba msimu uliopita ilimsajili Haruna Niyonzima kutoka Yanga na Yanga ilimsajili Ibrahim Ajibu kutoka Simba wakiwa na mategemeo makubwa ya kufanya vizuri katika ligi lakini wachezaji hao wakuweza kuzisaidia klabu zao kwa kiwango ambacho kilitarajiwa.

Ajib alimaliza msimu akiwa na magoli 7 pekee huku Haruna Niyonzima akicheza katika mzunguko wa kwanza wa ligi pekee baada ya kuumia katika mzunguko wa pili

chanzo eatv
21 July

USAJILI WA CHRISTIANO RONALDO NEEMA KWA CHELSEA

Usajili wa  Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid kwenda Juventus unaonekana kuwa neema kwa club ya chelsea kutokana na tetesi za usajili wa Gonzalo Higuai
USAJIRI WA CHRISTIANO RONALDO

Usajili wa  Christiano Ronaldo kutoka Real Madrid kwenda Juventus unaonekana kuwa neema kwa club ya chelsea kutokana na tetesi za nyota Gonzalo Higuain wa juventus kuonesha nia ya kusaini chelsea.

Usajili wa christian ronaldo ambaye ni nahodha wa Ureno aliyejiunga na Juventus kutoka Real Madrid kwa ada karibu £ 105 milioni wiki iliyopita.

Juventus sasa inaendelea na jitihada za kutafuta fedha baada ya kutoa dau kubwa kwenye usajili wa nyota wa zamani wa Manchester United.

Higuain ameidhibitishoia Sky Sports ripoti kuwa kuna mawasiliano kati ya makundi mawili.

Higuian anamjua meneja mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri kwani wamecheza msimu mmoja  huko Napoli miaka miwili iliyopita.

Akizungumzia jinsi Chelsea ingeweza kufaidika kutokana na safari ya Ronaldo, mtayarishaji wa Michezo, Keith Downie, alisema,   

"natarajia kuondoka Juve msimu huu.hivyo inaonekana anao mpango wa kujiunga na chelsea.

"Higuain alicheza kwa msimu mmoja wa mafanikio chini ya Maurizio Sarri

Higuain alimaliza kama mfungaji bora wa Serie msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa Argentina alifunga mabao 23 katika michezo 50 kwa Juventus katika mashindano yote msimu uliopita.

Friday, 20 July 2018

20 July

MBAPPE AZIDI KUITEKA REAL MADRID KUELEKEA PENGO LA CR7

Mbappe anaen­delea kutajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaowaniwa kwa uka­ribu na wababe wa Ulaya,Madrid walio na pengo kubwa la cr7
Mbappe 

 Mbappe anaen­delea kutajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaow aniwa kwa uka­ribu na wababe wa Ulaya, Real Madrid licha ya mche­zaji huyo kusisi­tiza kuwa hana mpango wa ku­hama kutoka Paris Saint-Ger­main (PSG) kwa sasa.

Mbappe mwenye miaka 19 alifunga goli la nne la Ufaransa walipoichapa Croatia 4-2 fanali ya Kombe la Dunia Moscow, pamoja na kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo katika michuano hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain Mbappe ndiye mchezaji wa pili asiyetimiza miaka 20 kutikisa wavu kwenye fainali ya Kombe la Dunia tangu Pele mnamo 1958.

Mbappe al­ionyesha kiwango cha juu akiwa na Ufaransa ka­tika Kombe la Dunia na kui­wezesha timu hiyo kubeba ubingwa, ame­kuwa akipigi­wa debe kwa kiasi kikubwa k u s a j i l i w a na kuoneka­na anafaa kuibeba Ma­drid baada ya kuondoka kwa Ronaldo.

Tangu Kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kwenda Juventus, Madrid au Los Blancos wamekuwa wakipambana sokoni kuhakikisha wanafanya usajili wa staa mkubwa kama ili­vyo kawaida yao kwa ajili ya kuziba pengo hilo.

Taarifa za ndani ya Madrid zi­naeleza kuwa Mbappe ambaye ana umri wa miaka 19 bado anaoneka­na kuwa ni chaguo sahihi na ndiyo maana mabosi wanahaha kuhak­ikisha wanalifanikisha hilo.

Mbappe anazidi kupata Sifa  nyingi ambazo zi­nambeba chipukizi huyo kusajiliwa ikiwemo kuonyesha makali akiwa na umri mdogo kuanzia ngazi ya klabu hadi timu ya taifa.

Kingine kuhusu Mbappe ni uwezo wake wa kufun­ga, amekuwa akionyesha makali katika ufungaji licha ya kuwa siyo straika halisi, kazi yake imekuwa nzuri licha ya kuwa amekuwa kati­ka kikosi kimoja na mastraika halisi wenye uwezo wa juu.

Hiyo inanogesha kwa kuwa in­aonekana kama anafuata nyayo za Ronaldo ambaye naye alikuwa winga lakini mwenye uwezo mkubwa wa kufunga.

Kibiashara pia nyota huyo anaonekana kuwa vizuri kwa kuwa hadi sasa sura yake imekuwa na soko kubwa PSG, hivyo upande mwingine Madrid wanaamini bi­ashara itakuwepo wakimsajili.
20 July

TETESI ZA SOKA LEO IJUMAA YA TAREHE 20 JULY 2018

Tetesi za soka leo zina angazia Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 31, atakayesalia na kupigania nafasi yake ya kwanza katika klabu ya Real hata iwapo klabu hiyo ya Uhispania itamsajili Courtois. (AS)
Tetesi za soka leo july 20, 2018

Tetesi za soka leo zina angazia Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 31, atakayesalia na kupigania nafasi yake ya kwanza katika klabu ya Real hata iwapo klabu hiyo ya Uhispania itamsajili Courtois. (AS)

Beki wa Juventus na Itali Daniele Rugani, 23, atajiunga na Chelsea katika kandarasi ya miaka mitano yenye thamani ya £77,000 kwa wiki. Huku Chelsea ikikubali kuwalipa mabingwa hao wa Itali dau la £44.2m. (London Evening Standard)

Mourinho: Natumai Pogba anaelewa kwanini alicheza vizuri Urusi
Leicester City imekubali malipo ya £12.5m na Liverpool kumnunua kipa wa Liverpool Dany Ward 25. Leicester City itakutana na mchezaji huyo wa Wales katika kipindi cha saa 24 zijazo.


Ward anatahitajika na mkufunzi wa Leicester Claude Puel ili kumpatia ushindani mkali kipa wa Denmark Kasper Schmeichel. (Daily Telegraph)

Valencia inajiandaa kumsaini beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah,20, kwa mkopo kabla ya kumpatia mkataba wa kudumu. (Super Deporte).

Fulham imeimarisha ombi lao la kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania David Lopez, 28, kutoka dau la £13.41m hadi £17.88m. (El Mundo).

Mchezaji mpya wa Liverpool na Uswizi Xherdan Shaqiri, 26, hakuonekana katika harakati za kuepuka kushushwa daraja kwa Stoke , kulingana na kiungo wa kati wa klabu hiyo Charlie Adam. (Talksport)

Je klabu yako inacheza mechi zipi za kirafiki kabla ya msimu kuanza?

Tetesi za soka leo pia zinaeleza kuwa klabu Swansea City imeanza mazungumzo na kiungo wa kati wa Manchester City kutoka Kosovo Bersant Celina katika mkataba wenye thamani ya £4m. (Daily Mirror)

Mshambuliaji wa United na Wales Ched Evans, 29, ananyatiwa kwa mkopo na klabu ya Fleetwood Town. (@SUFC_tweets)

Stoke City wanakaribia kuweka makubaliano ya dau la £10m na Huddersfield Town kwa winga wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 Tom Ince. (Daily Telegraph)

Klabu hiyo pia inakaribia kuthibtisha wachezaji wapya-Beki wa Aston Villa na Wales James Chester, 29, na kiungo wa kati wa West Brom na Ireland James McClean, 29. (Stoke Sentinel)

Tetesi za soka leo zinaeleza kuwa Manchester City itamuuza mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling katika kipindi cha miezi 12 ijayo iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hatokubali masharti mapya ya kandarasi yake .

Kandarasi ya mechezaji huyo inakamilika mwezi June 2020 lakini City haitakubali kuruhusu mchezaji wake yeyote muhimu kukamilisha kandarasi yake.. (Daily Mirror)


 Lakini Sterling anahofia kwamba fursa yake ya kuandikisha mkataba mpya na mabingwa hao wa ligi ya Uingereza imepungua kufuatia mchezo wake wa kiwango cha chini katika kombe la dunia msimu huu..(Daily Telegraph)

Aliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger analengwa na shirikisho la soka nchini Japan kuchukua wadhfa wa mkufunzi mpya wa timu ya taifa. Raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa bado ana hamu ya kuendelea na ukufunzi.. (Daily Mail)

Oxlade-Chamberlain kukosa kipindi kirefu cha msimu mpya
Chelsea imemuorodhesha kinda wa miaka 19 kutoka klabu ya AC Milan na kipa wa Itali Gianluigi Donnarumma. Katika orodha ya wachezaji wanaolengwa iwapo kipa wa Ubelgiji Thibaut Courtois,26, anayenyatiwa na Real Madrid ataondoka Stamford Bridge msimu huu. (London Evening Standard)20 July

MENEJA WA BAYERN MUNICH ATOA HATIMA YA RODRIGUEZ


Meneja wa Bayern Munich, Niko Kovac, amesema wazi kwamba klabu hiyo haina nia ya kukata mkataba wa miaka miwili kwa James Rodriguez, hivyo tiari amempa mkono wa kwaeli kurudi Real Madrid.
Meneja wa Bayern Munich aeleza kuhusu hatima ya james rodriguez pichani
Meneja wa Bayern Munich, Niko Kovac, amesema wazi kwamba klabu hiyo haina nia ya kukata mkataba wa miaka miwili kwa James Rodriguez, hivyo tiari amempa mkono wa kwaeli kurudi Real Madrid.

Mpango huo ulikuwa na chaguo la ununuzi kwa mwaka 2019.

Rodriguez anakwenda kustawi zaidi katika uwanja wa Allianz, na kuwa  wale wa Santiago Bernabeu wanatamani kumrudisha Hispania.
SOMA ZAIDI.......MOURINHO AMFUNGUKIA POGBA

Meneja wa Bayern Munich, Kovac aliwaambia waandishi wa habari alipoulizwa tena juu ya hatima ya James: "Ninajua tu kuwa tunao mpango wa mkopo ambao ni  halali juu yake.

Meneja wa Bayern Munich, ameendelea kusema "itafamika kama tutakaa naye kwa muda mrefu au ikiwa tutachukua chaguo  kudumu itafahamika pia. 


Alimalizia kwa kusema "tunajua pia kuna uvumi mwingi  unaendele katika vyombo vya habari."
20 July

MOURINHO AMFUNGUKIA POGBA

Mourinho adai pogba anaelewa kilichomfanya kufanya vyema kombe la dunia
Mourinho adai pogba anaelewa kilichomfanya kufanya vizuri katika kombe la dunia

 Mourinho kocha mkuu wa club ya Man United amesema ana matumaini kuwa mchezaji wake kutoka ufaransa Paul Pogba anaelewa kuhusu ni kwanini alicheza vizuri zaidi wakati wa mechi za Kombe la Dunia.

Kiungo hiyo wa safu ya kati wa Red Devils alifunga wakati Ufaransa waliishinda Croatia mabao 4-2 na kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya pili.

Mourinho alisema Pogba mwenye miaka 25 alionyesha mchezo mzuri sana kwenye mechi tatu za mwisho nchini Urusi.

"Ni yeye mwenyewe kufahamu ni kwa nini alicheza vizuri, hasa wakati wa awamu ya pili ya mashindano," alisema Mourinho.

Pogba alijiunga na United kwa pauni milioni 89 mwezi Agosti mwaka 2016, lakin akawa anachwa nje wakati wa mechi za msimu wa mwaka 2017-2018.

Aliachwa nje ya kikosi cha kwanza katika mechi zote wakati wa awamu za timu 16 za mwisho ambapo United ilishindwa na Sevilla.

Baada ya ushindi wa Ufaransa wa siku ya Jumapili beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand alisema "ni jukumu la Mourinho kumleta Pogba aliyekuwa kwenye Kombe la Dunia, alipitia mitihani migumu kwenye safu ya kati.

Huku Red Devil ikisafiri kwenda Marekani kwa safari ya maandalizi Pogba amebaki kupumzika.

Mourinho akizungumza  huko Los Angeles,  alisema, "nilimfanyia Pogba kile nilichowafanyia wachezaji wengine.

Nilituma ujumbe mzuri kabla ya Kombe la Dunia na wakati wa Kombe la Dunia sikumsumbua yeyote, Walihitaji kuangazi tu kazi ya timu zao za kitaifa.

Mourinho alisema kipa David de Gea, kiungo wa kati Nemanja Matic na mchezaji mpya Fred watajiunga na kikosi hicho wiki ijayo.

Mshambuliaji Alexis Sanchez kujiuanga kwenye ziara hiyo baada ya kukosa kupata visa.

Chanzo. Bbc swahili

Tuesday, 17 July 2018

17 July

AJIRA ZA  WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI , 2018

Ajira za walimu wa shule za msingi  na sekondari zilizotolewa julai mwaka huu  jumla ya Walimu 4,840 waliopangiwa vituo vya kazi kwenye Shule mbalimbali za Msingi na baadhi kwenye Shule za Sekondari nchini.
Ajira za walimu wa shule za msingi  na sekondari zilizotolewa julai mwaka huu

Ajira za walimu wa shule za msingi  na sekondari zilizotolewa julai mwaka huu  jumla ya Walimu 4,840 waliopangiwa vituo vya kazi kwenye Shule mbalimbali za Msingi na baadhi kwenye Shule za Sekondari nchini.

Ajira za Walimu hizo zilizotolewan zinawataka walimu waliopangiwa vituo vya kazi kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri zilipo shule walizopangiwa na baadaye kuripoti kwenye Shule walizopangiwa. Walimu wote wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 23 Julai, 2018 hadi tarehe 7 Agosti, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo:

(i) Vyeti halisi vya taaluma vya Kidato cha Nne na/au Kidato cha Sita;

(ii) Vyeti halisi vya kitaaluma vya mafunzo ya Ualimu katika ngazihusika; na

(iii) Cheti halisi cha kuzaliwa. Walimu wote waliopangiwa vituo vya kazi wanaelekezwa kuwa:

Vituo vyao vya kazi ni Shule ya Msingi au Sekondarializopangiwa na sio Makao Makuu ya Halmashauri; Anuani ya Simu “TAMISEMI” DODOMA Simu Na.: (026) 2333848, 2321607  2322853, 2322420 Nukushi: (026) 2322116, 2322146  2321013 Barua pepe: ps@tamisemi.go.tz Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Barabara ya Mlezi, S.L.P. 1923, DODOMA.

Mwajiriwa atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kasha akaondoka katika kituo chake cha kazi alichopangiwa Serikali itamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo; na
Hakuna Mwalimu atakayekubaliwa kubadilisha kituo kwa sababu yoyote ile. Kila mwajiriwa mpya anapaswa kuripoti katika kituo chake alichopangiwa na si vinginevyo.

Ajira za walimu wapya zinaambatana na sharti kuwa ambao watashindwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa nafasi zao zitachukuliwa na Walimu wengine 5,220 wenye sifa waliokosa nafasi.

TAARIFA YA SERIKALI KWA AJIRA MPYA 6180 PAMOJA NA VIGEZO HUSIKA BOFYA HAPA
Wakurugenzi wa Halmashauri husika wawapokee Walimu waliopangwa kwenye Halmashauri zao kwa kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya kuripoti kwao.

Taarifa ya kuripoti waajiriwa hao itumwe Ofisi ya Rais- TAMISEMI ifikapo au kabla ya tarehe 10.08.2018 baada ya tarehe ya mwisho ya kuripoti. Majina ya Walimu waliopangiwa vituo yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA YA AJIRA ZA AJIRA