BADNEWS; HII HAPA TAARIFA YA TANZIA YA MAPACHA WALIOUNGANA - EDUSPORTSTZ

Latest

BADNEWS; HII HAPA TAARIFA YA TANZIA YA MAPACHA WALIOUNGANA

maria na consolata mapacha walioungana waliopatwa na mauti siku ya leo .BADNEWS; HII HAPA TAARIFA YA TANZIA YA MAPACHA WALIOUNGANA
😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢
Mapacha walioungana (Maria na Consolata) wamefariki dunia usiku huu wa Jumamosi Juni 2, 2018 katika hospitali ya Iringa walikokuwa wakitibiwa.

Mapacha Hawa walifanikiwa kuanza masomo yao ya juu katika Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu) cha mjini Iringa mwaka jana.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa, Richard Kasesela amethibitisha kupkoea taarifa za msiba huo.


Mapacha hao waliwahi kulazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu wakitolewa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa.


Maisha ya Maria na Consolata

Maria na Consolata Mwakikuti walizaliwa eneo la Ikonda, wilaya ya Makete kusini magharibi mwa Tanzania mwaka 1996.

Walisoma shule ya msingi ya Ikonda kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Maria Consolata na baadaye wakasomea hadi kidato cha sita katika shule ya Udzungwa wilaya ya Kilolo.

Septemba mwaka jana, baada ya kufaulu mtihani wa kidato cha sita, walijiunga na chuo kikuu cha kikatoliki cha Ruaha, Iringa.

Walianza kuugua maradhi ya moyo na Desemba wakahamishiwa taasisi ya maradhi ya moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako walilazwa kwa miezi miwili.
Walipofaulu mtihani wa kidato cha sita, walieleza furaha yao kuu baada ya kufaulu mtihani na kueleza ndoto zao.

"Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana," alieleza Consolata.

Walieleza sababu za kuchagua chuo cha Ruaha kwenye mkoa waliokuwa wanaishi tofauti na vyuo vingine au kama ilivyo kwa wanafunzi wengine ambao hupenda kubadili mazingira.

"Kwanza tunapenda mazingira ya Iringa, hatukutaka kwenda Dar es Salaam kwa sababu ya kwanza tunapenda kuishi pamoja na walezi wetu Masista waliokuwa wanatulea tukiwa wadogo na pili mikoa mingine ni mbali na tunapoishi. Pia ni kwa sababu kwa hali yetu tulivyo hatumudu kuishi kwenye mazingira ya joto. Mji wa Iringa ni baridi, hali hii tumeizoea.''

Maria na Consolata walikuwa wamewahimiza wazazi kuwajibika ipasavyo kwa watoto wao wenye ulemavu wakisema hakuna lisilowezekana.

"Wazazi washukuru Mungu kupata watoto wenye changamoto kama wao wasione kuwa na mtoto mlemavu ni laana. Pili wawaone kama watoto wengine na kuwapa mahitaji yao ya msingi, wawawezeshe, wawapatie nafasi ya kujiendeleza maana wakiwezeshwa wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri.''

EDUSPORTSTZ ina toa pole kwa familia ya maremu na taifa kwa ujumla
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.