Type something and hit enter

On
Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Christiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 anataka kuichezea Manchester United na atakubali kurudi Old Trafford, kulingana na kocha wa zamani wa Uingereza na Real Madrid Fabio Capello. (Goal.com).John Terry anatarajiwa kuunganishwa tena na mchezaji mwenza wa Uingereza na Chelsea Frank Lampard katika klabu ya Derby, baada ya Lampard kuajiriwa kama mkufunzi wa kikosi hicho cha ligi hiyo ya mabingwa. Beki Terry, 37, alitoka Aston Villa baada ya klabu hiyo kushindwa kufuzu katika ligi ya Uingereza ya Premier League. (Star)

Mchezaji wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 24, amekubali kandarasi ya miaka minne na klabu ya Juventus na atafanyiwa ukaguzi wa matibabu na mabingwa hao wa Itali.(Calciomercato)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kukutana na mamake Ousmane Dembele katika juhudi za kumshawishi mchezaji huyo wa Barcelona na Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 kuhamia Anfield msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester United ina hamu ya kumsaini Gareth Bale msimu ujao lakini hawajapata ishara yoyote kutoka kwa Real Madrid iwapo klabu hiyo inataka kumuuza mchezaji huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 28. (ESPN)

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann anasema kuwa ataamua hatma yake kabla ya kombe la dunia huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akihusishwa na uhamisho wa Barcelona. (FourFourTwo)

Mkufunzi wa zamani wa Ufaransa na Paris St-Germain Laurent Blanc ni miongoni mwa wagombea wakuu wa wadhfa wa ukufunzi katika klabu ya Chelsea pamoja na mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri. (Sun)

Everton inaongoza kundi moja la vilabu vya Uingereza katika harakati za kumsaini kinda wa Norwich na Uingereza mwenye umri wa miaka 21 kiungo wa kati James Maddison, ambaye alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka katika klabu yake msimu uliopita .(Sky Sports)

Mkufunzi mpya wa klabu ya West Ham Manuel Pellegrini atamsaini beki wa Fulham Ryan Fredericks, 25, wiki ijayo baada ya kukubali kutia saini kandarasi ya miaka minne na raia huyo wa Uingereza (London Evening Standard)

West Ham pia wameanza mazungumzo ya kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Argentina mwenye umri wa miaka 28 Javier Pastore katika mkataba utakaogharimu dau la £17m deal. (Sky Sports)

Winga wa Leicester Riyad Mahrez amejitokeza katika picha ambazo amevalia jezi mpya ya klabu hiyo akiongeza matumaini miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anayesakwa na Manchester City kwa dau la £60m atasalia na klabu hiyo. (Sun)

Roma wanafanya mpango wa kumuuza kipa wao raia wa Brazil Alisson 25, ambaye analengwa na Liverpool na badala yake kumnunua kipa wa klabu ya Bayer Leverkusen na Ujerumani Bernd Leno, 26. (Corriere dello Sport - via Metro)

Aston Villa itahitaji £40m kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish, 22, huku kukiwa na hamu kutoka kwa Leicester. (Sky Sports)

Manchester City ina mpango wa kumnunua beki wa Valencia na Ureno Joao Cancelo, 24. (Manchester Evening News)

Beki wa Juventus na Itali Giorgio Chiellini, 33, anatarajiwa kusaini kandarasi mpya itakayomuweka katika klabu hiyo ya Serie A hadi mwezi Juni 2020. (Football Italia)

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino na mwenzake wa Real Madrid anayeondoka Zinedina Zidane
Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa atasikiza ombi la Real Madrid iwapo wanamtaka kumrithi mkufunzi wa klabu hiyo anayeondoka Zinedine Zidane(Mirror)

Raia huyo wa Argentine ameionya miamba hiyo ya Uhispania kwamba mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs Daniel Levy, ambaye anajulikana kwa mazungumzo makali hatokubali .. (Marca)

Levy atakataa ombi lolote kutoka kwa Real Madrid kumchukua Pochettino msimu huu kulingana na mwandishi wa Uhispania na mtunzi wa kitabu kipya cha Pochettino Guillem Balague. (BBC Radio 5 live)

Jinsi Zidane alivyoishangaza Real Madrid-'Uamuzi wake ulikuwa kama mlipuko wa bomu'
Chelsea yasitisha ujenzi wa uwanja wake mpya

Sporting Lisbon inatafuta uhamisho wa William Carvalho, huku Everton ikidaiwa kumnyatia kiungo huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 26 (Sky Sports)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen anadai kuwa vilabu kadhaa vina hamu ya kumsaini mchezaji huyo wa Denmark . (London Evening Standard)EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment