;
HISTORIA "CHANZO CHA UHASIMU KATI YA MAN UNITED vs LIVERPOOL - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 2 June 2018

HISTORIA "CHANZO CHA UHASIMU KATI YA MAN UNITED vs LIVERPOOL


Mshabiki wa kweli wa Manchester United huwezi kuipenda Liverpool na kitu chao chochote kinachohusiana nacho.Manchester United huwa hatuna huruma na Liverpool hadi kufa.Unajua chanzo cha chuki kilianzia wapi?.

Ilianza tarehe 2 February mwaka 1958 ambapo wachezaji wa Manchester United walipata ajali ya ndege na kupoteza maisha.
Liverpool walileta kejeli sana baada ya huu msiba mpaka wakaamua kutengeneza nyimbo ya kuwakejeli Manchester United na wakiimba "Your players have turned manure"Wakimaanisha wachezaji wenu waliokufa wamegeuka mbolea.

Watu wanapenda sana kuwakejeli mashabiki wa Manchester United kwa kupitia hili neno "MANURE"Kila mtu anayetukejeli Manchester United kwa kupitia hili neno huwa ananikumbusha hii ajali ya ndege maana chimbuko la hili neno lilianzia huko.

Ilikuwa ni huzuni sana kipindi hiko hila wao Liverpool hawakujali waliendelea kushangilia kwa furaha huu msiba.Na kwa nini mashabiki wengi wa Manchester United duniani huwa wanaipenda Real Madrid kama timu yao ya pili?

Ni kwa sababu hii hapa baada ya ajali ya ndege mwaka 1958 mwaka huo huo Real madrid walikuwa mabingwa wa Uefa champion league na waliomba kombe hilo wapewe Manchester United kama kuwafariji hila Manchester United walikataa kupewa kitu cha bure ambacho hawajakitolea jasho.Real madrid hawakuishia hapo wakati ligi imeisha na likizo imeanza waliwalika Manchester United nchini Hispania na gharama zote waligharamia wao.

Kule nchini Hispania Real madrid waliandaa mechi za kirafiki nyingi tu na waliomba hayo mapato yote wapewe Manchester United hili yawasaidie kujijenga upya.Real madrid hawakuishia hapo waliamua kumtoa mchezaji wao bora Alfredo De Steffano bure achezee Manchester United.

Alfredo De Stefano alikuwa mmoja wa wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwa Manchester United mpaka wakachukua kombe lao la kwanza la Uefa champion league akiwa anakaribia kustaafu.

Kwa hiyo uhusiano wa Manchester United na Real madrid ni mkubwa na hauwezi kuvunjwa hata kama Ramos angeng'oa bega la Salah fainali.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB