HESLB KUSITISHA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA DIPLOMA KUANZIA MWAKA 2018/19 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 3 June 2018

HESLB KUSITISHA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA DIPLOMA KUANZIA MWAKA 2018/19

HESLB

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesitisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma stashahada (diploma) kuanzia mwaka wa masomo 2018/19 kama ilivyotangaza awali.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Juni 3, 2018 kupitia taarifa ya bodi hiyo iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wake, Abdul Razaq Badru.

Taarifa hiyo inasema hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha kiasi chote cha Sh427.5bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2018/19 zinaelekezwa kwa wanafunzi wenye mikopo hivi sasa na waombaji wapya, wahitaji ambao wana sifa za kujiunga na kozi za shahada tu ambao ndio walengwa wakuu.

“Tunatoa wito kwa wanafunzi wote wenye sifa za kujiunga na masomo ya shahada katika taasisi za elimu ya juu na ambao ni wahitaji wa mikopo kuhakikisha wanasoma kwa makini mwongozo wa utoaji mikopo na kuuzingatia. Mwongozo unapatikana katika tovuti ya HESLB,” inaeleza.

Taarifa hiyo inafafanua kuwa kwa takwimu za mwaka 2017/18, takribani maombi 10,027 ya mikopo yaliyowasilishwa HESLB yalikuwa na upungufu kama kutosainiwa, kutokuwa na viambatanisho sahihi na mambo mengine.

Mei 10, 2018 bodi hiyo ilitoa mwongozo unaosimamia utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/19, mwongozo huo pamoja na mambo mengine, unaeleza kuwa bodi hiyo itaanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na kuwa mwongozo kuhusu utaratibu wa kuomba mikopo hiyo ya wanafunzi wa stashahada ungetolewa baadaye. 


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ