BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 11 June 2018

11 June

MAGAZETI YA LEO TANZANIA NA ULAYA SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 11 JUNE 2018

Kama kawaida Edusportstz tayari imeshakusogezea stori kubwa zilizotengeneza headline katika kurasa za mbele na nyuma za Magazeti ya Tanzania jumatatu ya leo JUNE 11/2018. Chukua time yako kwa kupitia Stori zote kali za udaku, siasa, michezo, burudani na mambo mengine mbali mbali.

MAGAZETI YA LEO TANZANIA NA ULAYA SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 11 JUNE 2018EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Sunday, 10 June 2018

10 June

SIMBA YATAFUNWA BILA HURUMA

 
Klabu ya Gormahia ya nchini Kenya imefanikiwa kuchukua ubingwa wa michuano ya Sportpesa kwa kuifunga klabu ya Simba ya Tanzania goli 2-0.
Wachezaji wa Klabu ya Gormahia ya nchini Kenya wakishangilja kuchukua ubingwa wa michuano ya Sportpesa baada ya  kuifunga klabu ya Simba ya Tanzania Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Gor Mahia walitawala zaidi mchezo wakiwa na kikosi chao kamili huku Simba wakipata wakati mgumu kutengeneza nafasi za kufunga. 
Gor Mahia wamejipatia mabao yao kupitia kwa Mshambuliaji wao hatari, Medy Kagere aliyefunga la kwanza katika dakika ya 6 tu ya mchezo na kufanya kipindi cha kwanza kiende kwa bao 1-0. 
Kipindi cha pili kilianza tena kwa Gor Mahia kuzidi kulisakama lango la Simba wakionesha njaa ya kupata goli jingine ambapo mnamo dakika ya 54, Tuyisenga alifunga bao la pili kwa kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka kulia mwa Uwanja na kumuacha Kipa Aishi Manula akiwa hana cha kufanya.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Gormahia kuchukua ubingwa huo baada ya mwaka jana kuchukua ubingwa huo ambao mashindano yake yalifanyika nchini Tanzania.

Gormahia wamejikatia tiketi ya kwendaGoodison Park nchini uingereza kucheza dhidi ya Everton.

Mchezo huo umekamilika kwa mabao 2-0 


Chanzo: Mtila blog
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ
10 June

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA NACTE NA GUIDEBOOK KWA UDAHILI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2018/2019

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi katika Vyuo Visivyokuwa Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki vinavyotoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada nchini. Jukumu mojawapo la Baraza, ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo  vya Elimu ya Ufundi yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
nembo ya nacte

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA NACTE NA GUIDEBOOK KWA UDAHILI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2018/2019
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi katika Vyuo Visivyokuwa Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki vinavyotoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada nchini. Jukumu mojawapo la Baraza, ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo  vya Elimu ya Ufundi yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kufahamisha umma kuwa 


Udahiliwa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote isipokuwa za Ualimu umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 8 Juni, 2018 na utaendelea hadi tarehe 8 Septemba, 2018 kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo katika ngazi hizo.Maelekezo ya Udahili kwa kada za Ualimu yatatolewa baadaye.

Hivyo wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kutuma maombi moja kwa moja vyuoni ili kuweza kupata nafasi ya kujiunga na mafunzo kwa mwaka wa masomo wa 2018/2019. Aidha kwa wanaoomba udahili katika vyuo vya serikali vinavyotoa kozi za Afya wanaweza pia kuanya hivyo kupitia tovuti ya www.nacte.go.tz

Pia Baraza linawashauri waombaji na wazazi/walezi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye Vyuo vinavyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa mwaka wa masomo 2018/2019 (Admission Guidebook for 2018/2019 Academic year).

Mwongozo wa Udahili unapatikana katika tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz)

Kuona Mwongozo wa udahili kwa mwaka 2018/2019 (Admission Guidebook 2018/2019) bonyeza hapa


IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 8/06/2018

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Saturday, 9 June 2018

09 June

MSWALI MUHIMU YA MASHABIKI WA YANGA KWA KARIA


Baaada ya kuwepo kwa taarifa ya kwamba yanga hawatashiriki mashindano ya kagame cup ,raisi wa tff wallace karia amewapa timu ya yanga masaa 48 ya kujitakari na maamuzi yao hayo.

Edusporttz ilifafanya mahojiano na mashabiki wa yanga kadhaa na walitoa maoni kama ifuatavyo:-


 1. azam anaingia kama bingwa mtetezi ,simba bingwa wa nchi ,je yanga anaingia kama nani kwenye mashindano haya? kama mualikwa je hana haki yabkujitoa?

2.  Kwanini haya mashindano hayakuwepo kwenye ratiba ya tff ya mwaka?  kwa hiyo ni dhahiri yanga wanayo sababu

 3. Kama makundi ya kagame yapo matatu na timu kutoka bara zipo tatu kulikuwa na ulazima gani simba na yanga kuwa kundi moja? au kuna nn nyuma ya pazia?

4. yanga wametoa sababu ya kwamba wachezaji wengi wamepitia majeruhi ya muda mrefu halafu pia wana michuno ya shirikisho afrika kwanini karia unaipinga sababu hii wakati wewe ni raisi wa tff na haya yote ulikuwa unayaona?  halafu raisi wa tff unatoa majibu kwa kufananisha na rayon sports na gor mahia je wao wamepitia magumu kama ya yanga?

5. Wachezaji wa yanga hawakupata muda kabisa wa kupumzika kwenye ratiba ya mwisho ya ligi huku wakisafiri kila kukicha na wapangaji wa ratiba walikuwa tff hawaioni kama hii ni sababu pia ukizingatia wachezaji ni binadamu wanahitaji kupumzika?

6. Je yanga wakipeleka under 20 cecafa watakubali?

 7. kwani karia ndio raisi wa cecafa mpaka ailazimishe yanga kucheza michuano hiyo?? 

8. Mimi nilizani karia atakuja na vifungu vya kanuni na sheria vinavyowabana yana washiriki kagame cup mwaka huu


WENGI WANAHOJI KUNA NINI NYUMA YA PAZIA?
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
09 June

MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUNE 9, 2018


Kama kawaida Edusportstz tayari imeshakusogezea stori kubwa zilizotengeneza headline katika kurasa za mbele na nyuma za Magazeti ya Tanzania jumamosiya leo JUNE 9/2018. Chukua time yako kwa kupitia Stori zote kali za udaku, siasa, michezo, burudani na mambo mengine mbali mbali. 

Friday, 8 June 2018

08 June

RASMI YANGA KUTOSHIRIKI KAGAME SABABU HII HAPA


klabu ya yanga ambayo haikuwa na msimu mzuri wa ligi pamoja na mashindano aliyoshiriki mwaka huu, kumekuwepo na taarifa kwamba wanakwenda kwenye mkutano mkuu ambao baadhi yao wanauita wa mabadiliko kwa klabu hiyo.

mapema wiki hii kulitoka ratiba ya michuano iliyopo chini ya cecafa ikishirikisha timu kutoka afrika mashariki na kati ambapo yanga alikuwa kwenye kundi moja na mtani wake simba.

Leo kumetoka taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari kwamba yanga haitashiriki michuano hiyo kwa sababu mbalimbali.

Sababu hizo ni timu kuwa katika mashindano mengi na wachezaji kukosa muda wa kupumzika, baadhi ya nyota wake kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu sababu ya majeraha, Kuipa timu nguvu kuangalia zaidi mashindano ya CAF confederation.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
08 June

KAULI TATA YA MANJI KUELEKEA MKUTANO MKUU WA YANGA


Kuelekea mkutano mkuu wa yanga wanachama,mashabiki na viongozi wanaonekana kuwa na wazo la mabadiliko kwenye klabu yao kutokana na hali ya klabu kwa sasa jinsi ilivyo.

Viongozi wengi wameachia ngazi zao kabla ya mkutano huo.

kumekuwepo na taarifa ya kwamba huenda Mwenyekiti aliejiudhuru wa klabu hiyo Yusuph manji akarudi kwenye timu hiyo kwa mara nyingine.

Kuelekea mkutano huo Yusuph maji ametoa kauli tata kama atahitajika kurudi kwenye klabu hiyo.

Yusuph manji alisema "Yanga ni klabu yetu sote na binafsi hii ni kama sehemu ya familia yangu. Kuona klabu inasuasua kiasi hiki sifurahi, wapo waliotufikisha hapana lazima wawajibike kwa mizani ya uongozi bora ili sote tuungane kuijenga upya klabu katika misingi bora na endelevu.
 Misingi endelevu ili yeyote yule mwenye mapenzi mema na klabu weledi katika uongozi aweze kuiongoza ,binafsi sona pingamizi kurejea endapo watawajibika waliotuvuruga, wanachama kuridhia kuijenga yanga upya yenye mtazamo chanya wa kimaendeleo pamoja na miundo mbinu"

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ