UNAI EMERY ATAFUTA KIU YA MASHABIKI WA ARSENAL? - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD EDUSPORTSTS NEWS APP HAPA

Tuesday, 22 May 2018

UNAI EMERY ATAFUTA KIU YA MASHABIKI WA ARSENAL?


UNAI EMERY 
Baada ya miaka 22 mashabiki wa arsenal wameachiwa klabu yao na kocha wao wa muda arsene wenger ambae amedumu kwenye klabu hiyo toka mwaka 1996 ila 2018 ukawa mwaka wake wa mwisho kuwa pale Emirates, Huku kikombe cha EPL mara ya mwisho wakiwa wamekishangilia mwaka 2003.

Huku klabu ya Psg ilimalizana na kocha wake ambae amefanikisha kuchukua kombe la ligi kuu ufaransa msimu huu pamoja na kombe la ligi.

Ambapo kocha huyo mpaka sasa anapewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa wenger baada ya kocha huyo kukutana na uongozi wa arsenal.

Ila swali la kujiuliza "je atafuta machozi ya mashabiki wa arsenal?"

shida ya mashabiki wa arsenal ni kuchukua ubingwa wa EPL pamoja na kufanya vizuri champions league kitu ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu sana.


Unai emery ametoka kwenye klabu ya psg ambayo huwa ina matumizi makubwa sana ya fedha hasa katika kipindi hiki cha usajili na kuweza kushindana na timu yoyote ile duniani mfano aliweza kumng'oa Neymar kwa miamba ya katalunya kwa dau ambalo liliweka rekodi.

Lakini ameshindwa kuiletea Psg mafanikio katika champions league ambako kulikuwa ni malengo ya klabu.

Anakuja arsenal ambayo ni moja ya klabu ambazo haziamini katika matumizi makubwa ya pesa kwenye usajili je ataweza kuwabadili wachezaji waliopo na kuwa sehemu ya faraja kwa mashabiki wa arsenal au klabu itabadili mfumo na kwenda kushindana sokoni na klabu zenye uchu wa wachezaji.

Tulipe muda tutapata majibu lakini klabu ambayo imeishi kwenye falsafa ya mtu kwa miaka 22 ni ngumu kuitoa na kuiweka ya kwako.