Type something and hit enter

On

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya uchochezi.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amethibitisha kuachiwa kwa Viongozi hao wawili na tayari Sugu ameshafika nyumbani kwake.

Wengine waliofika gerezani kumpokea ni Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani, Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda.

Wawili hao wamepokelewa Uraiani leo Mei 10, 2018 asubuhi na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho waliosafiri hadi Mbeya kwa ajili ya mapokezi hayo.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment