MAREKANI ACHEZEA KICHAPO CHA 5-0 TOKA TANZANIA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD EDUSPORTSTS NEWS APP HAPA

Monday, 14 May 2018

MAREKANI ACHEZEA KICHAPO CHA 5-0 TOKA TANZANIA

kikosi cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu

Timu ya watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kutoka nchini Tanzania, imeifunga timu ya watoto kama hao kutoka nchini Marekani, jumla ya mabao 5-0 katika mashindano ya Street Children World Cup na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.

Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Street Child United, timu ya wasichana ya Tanzania imefanikiwa kutinga hatua hiyo ya nusu fainali, ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja naikiwa haihafungwa goli hata moja, na kuweka rekodi ya kipekee.

Mchezo wa timu ya Tanzania dhidi ya Marekani, umefanyika katika Uwanja wa Timu kubwa ya Soka ya Lokomotive Moscow jijini Moscow nchini Urusi ambapo mshambuliaji wa Tanzania, Yasinta Peter anaongoza kwa kufunga magoli mengi zaidi, ambapo mpaka sasa amezifumania nyavu mara 5.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ