MANENO YA FREEMAN MBOWE KWA MBUNGE HECHE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 7 May 2018

MANENO YA FREEMAN MBOWE KWA MBUNGE HECHEMwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa kwa siku kadhaa zilizopita
amekuwa katika wakati mgumu na kushindwa kuelewa neno gani anaweza kumpa Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake Suguta ambaye alifariki kwa kuchomwa kisu na askari

Mbowe amesema kuwa kifo ambacho kilimpata mdogo wake na Heche kinaumiza sana ndiyo maana kwa siku kadhaa amekosa maneno mazuri ya faraja kumpa kiongozi huyo wa CHADEMA


"Ni siku ya 3 sasa toka ulimpozika mdogo wako, nimefikiria kwa muda mrefu, maneno gani nitumie kukupa pole lakini imeniwia vigumu sana kuyapata maneno hayo kutokana na aina ya kifo kilichokatisha maisha ya kijana mdogo kabisa katika Taifa. Tunafundishwa ya kwamba tushurukuru kwa yote,liwe baya au zuri, sawa tunashukuru lakini kwa kifo cha aina ya mdogo wako kinauma na kuumiza sana, bora mtu akiumwa inakuwa ni rahisi mnasema ni kazi yake Mungu hakuna anayeweza kuipinga na huwa ni kipindi kigumu kuliko wakati mwingine wote wote katika maisha yetu wanadamu pale tunapoondokewa na wapendwa wetu lakini kwa kifo cha aina ya mdogo wako ni maumivu zaidi"
Aidha Mbowe alitumia wakati huo kutoa pole kwa familia ya John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake huyo


"Nakupa pole sana Kamanda Heche John katika kipindi hiki kigumu, Mungu akupe nguvu wewe, familia, ndugu, jamaa na marafiki, pole kwa mara nyingine kamanda, apumzike kwa Amani Kamanda Suguta"
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ