Type something and hit enter

On

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameitaja mikoa ya Tanga,Mwanza na Dodoma kuwa ndiyo mikoa ambayo kiwango cha maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kinazidi kupanda. Akizungumza jana Mei 9,2018 wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa nne wa VVU na UKIMWI na sherehe za miaka 30 ya mpango wa taifa wa kudhibiti Ukimwi, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika chuo cha Mipango jijini Dodoma,Waziri Ummy alisema ipo haja ya wadau wote kushirikiana katika kuhakikisha maambukizi yanapungua.


Amesema maambukizi yanazidi kuongezeka katika mikoa 11 nchini ukiwemo mkoa wa Dodoma, Tanga na Mwanza licha ya kiwango cha maambukizi kitaifa kushuka kutoka asilimia 7 mwaka 2003/04,hadi asilimia 4.7 kwa mwaka 2016/17.


"Wakati maambukizi ya VVU yakipungua kitaifa lakini katika mikoa 11 yamepanda mfano Tanga ilikuwa na maambukizi kwa asilimia 2.4% lakini sasa ni 5% ,Dodoma 2.9% sasa ni 5% na Mwanza 4.2% sasa imekuwa 7.2 %",alieleza.


Naye Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amesema mpaka sasa serikali haijapata tiba ya virusi vya Ukimwi na Ukimwi licha ya kuanza majaribio ya dawa kinga. 


habari na Kadama Malunde - Malunde1 blog
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment