Type something and hit enter

By On
'
Fredie Blom anasema kuwa hakuna siri kuhusu maisha yake marefu
Fredie Blom alihudumu wakati mwingi kama mfanyikazi katika shamba na katika sekta ya ujenzi nyakati za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini lakini huenda hivi karibuni akatambuliwa kuwa mtu mzee zaidi duniani , kama anavyoripoti mwandishi wa BBC Mohammed Allie kutoka Cape Town.


Ijapokuwa aliwacha kunywa pombe miaka mingi iliopita , Fredie Blom ni mvutaji sigara wa mara kwa mara.

''Kila siku mimi huvuta sigara mara mbili au tatu, mimi hutumia tumbaku yangu kwa sababu sivuti sigara za kawaida. Shinikizo ya kutaka kuvuta sigara ipo juu''.

''Mara nyengine mimi hujiambia nitawacha lakini naona kana kwamba najidanganya. Kifua changu kinanishinikiza kuvuta hivybasi hulazimika kutengeza kiko changu cha tumbaku.Namlaumu shetani kwa hayo kwa kuwa ana nguvu sana''.

Tanzania: Wamiliki wa blogu, TV na redio mtandaoni watakiwa kujisajili
Raheem Sterling akemewa kwa kuchora tatuu ya bunduki mguuni
Washukiwa wa ufujaji wa pesa Kenya wafikishwa kortini
Umaarufu wake
Kitu kimoja kinachokugusa moyoni unapokutana na mzee huyo ni vile alivyoimarika kiafya na hali yake. Akiwa mrefu na mwenye nguvu anatembea bila usaidizi wowote mbali na kwamba hana ugonjwa wowote.

Mfanyikazi huyo wa zamani wa shambani ambaye alifikisha umri wa miaka 114 mwezi Mei tarehe 8 anasemekana kuwa mtu mzee zaidi aliyehai ijapokuwa hilo halijathibitishwa na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness.

Taji hilo lilikuwa likishikiliwa na mwanamke wa Jamaica Violet Moss Brown hadi tarehe 15 Sepetmba 2017 wakati alipofariki akiwa na umri wa miaka 117.

Kitabu cha Guiness cha rekodi za dunia kinasema kuwa bado kinatafuta ushauri kutoka kwa wataalam wa historia kuthibitisha ni nani anayeshikiia taji hilo la mwanamke mzee zaidi pamoja na lile la mwanamume mzee zaidi.

Kulikuwa na wasiwasi kuhusu maisha yake hadi alipotoa kibali chake cha kuzaliwa
Bwana Blom, mwenye masharubu na ndevu za kijivu hana siri yoyote kuhusu maisha yake marefu.

''Kuna kitu kimoja -Ni Mungu aliye juu mbinguni. Sina chochote ninaweza kuanguka muda wowote, lakini Mungu ananizuilia ,ana nguvu zote''', alipoulizwa ni nini haswa kinachomfanya kuendelea kuishi.

Nahisi vyema kabisa , niko shwari .Moyo wangu una nguvu lakini ni miguu yangu pekee ambayo imeanza kukubali uzee wangu -siwezi kutembea tena vile nilivyokuwa nikitembea, anazungumza kwa lugha ya Afrikaaner kwa sauti ya juu.

Amejipatia umaarufu ambao umewafanya raia pamoja na maafisa wa serikali wakiwemo mawaziri kumtembelea nyumbani kwake huko Cap Town.

Amesema kuwa ni hisia nzuri kujua kwamba watu wanakuthamini.

Katika siku yake ya kuzaliwa , duka moja la jumla na idara ya maswala ya kijamii serikalini ilimpatia keki kubwa.

Alifanya kazi hadi miaka ya 80
Janetta, ambaye ni mkewe bwana Blom kwa miaka 48 ambaye ni mdogo wake kwa miaka 29 anasema kuwa mumewe amekuwa na afya njema na alienda hospitalini mara moja pekee - miaka mingi iliopita wakati alipokuwa na tatizo la goti.

Anasema kuwa watu wengi awali walikuwa na wasiwasi kuhusu umri wa mumewe.

Kulikuwa na maswali kuhusu swala hilo wakati alipotuma ombi la kupata kitambulisho miaka kadhaa iliopita , lakini mpwa wake alienda mjini London ili kupata cheti chake cha kuzaliwa ambacho kilitoa thibitisho lililohitajika.

Sihle Ngobese , msemaji wa idara ya West Cape kuhusu muendelezo wa kijamii aliniambia kwamba ukweli kwamba serikali ilimpatia bwana Blom kitambulisho kilichorekodi siku yake ya kuzaliwa kuwa tarehe 8 mwezi Mei 1904 ni dhihirisho tosha.

Blom anakumbuka ujana wake akijaribu kuwinda ndege kwa kutumia manati
Alikuwa mdogo wakati bwana Blom alipoondoka Adelaide, mji mdogo mashariki mwa Cape Town kuelekea Cape Town.

Kwa kuwa hakuhudhuria masomo shuleni hawezi kusoma wala kuandika.

Badala yake macho yake hujifunga funga wakati anapofikiria ujana wake.

"Wakati nilipoamka alfajiri nilipenda kwenda nje na kuuangalia ulimwengu. Mara nyengine ningechukua manati yangu na kuwapiga ndege -nilihisi vyema wakati nilipoangalia ukanda wangu na ulikuwa umejaa ndege ambao nilikuwa nimewapiga.Mkewe aliniambia kwamba hali chochote maalum. Hupendelea kula nyama katika kila chakula lakini pia hula mboga nyingi.

Bwana Blom bado ana nguvu za kuosha nguo na kuvaa ijapouwa kulingana na mkewe hupata shida kuvaa viatu vyake. Mara nyengine hupendelea usaidizi wa mjukuu wake.

Kwa mtu ambaye alianza siku yake saa kumi na nusu alfajiri katika kipindi alichokuwa akifanya kazi , bwana Blom huamka kuchelewa na hafayi mambo mengi nyumbani.

''Siwezi kufanya chochote -siwezi hata kupanda ngazi tena . Mimi huketi tu. Sina muda na upuzi uliopo kwenye runinga''.

Anapendelea sana kuketi nje ya nyumba yake na kuvuta sigara

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment