SABABU ZA MAGEREZA KUACHIWA KWA SUGU NA MWENZAKE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD EDUSPORTSTS NEWS APP HAPA

Thursday, 10 May 2018

SABABU ZA MAGEREZA KUACHIWA KWA SUGU NA MWENZAKEJeshi la Magereza limeeleza kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiliwa huru kwa msamaha wa Rais uliotolewa katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Afisa Habari wa Jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo, Rais alitoa msamaha kwa wafungwa ambapo baadhi walitoka siku hiyo hiyo na wengine walibaki kumalizia muda wao, kutokana na kupunguziwa adhabu.

“Jumla ya wafungwa 585 kati ya 3,319 waliopewa msamaha waliachiliwa Aprili 26, mwaka huu. Wafungwa 2,734 akiwemo Sugu na Masonga walibakia gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya msamaha wa Rais Dkt John Pombe Magufuli”, amesema Mboje.

Wawili hao walikuwa katika Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi (5) baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya kumkashifu Rais Dkt. Magufuli ambapo hukumu yao ilitolewa Februari 26, 2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite baada ya na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mh Joseph Mbilinyi (SUGU) ameachiliwa huru leo Mei 10, na baada ya kuachiliwa kwake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema bado watakata rufaa kuhusu kesi hiyo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ