Type something and hit enter

On
 Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Soka ya Barcelona, Andres Iniesta (33) jana ulikuwa usiku wake baada ya kuwaaga rasmi wachezaji wenzake na uongozi wa klabu hiyo ikiwa ndiyo mwisho wake kuitumikia timu hiyo.
Tukio hilo lililohidhuriwa na wachezaji karibu wote wa Barcelona, lilifanyika katika mechi ya kufunga Msimu wa ligi Kuu ya Hispania Laliga 2017/18 ambapo barcelona waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad.

Mechi hiyo ambayo ilichezwa katika uwanja wa Camp Nou, nyumbani kwa Barcelona, ilihudhuriwa na mashabiki zaidi ya 90,000.


Kiungo huyo raia wa Uhispania aliyeichezea klabu hiyo kwa miaka 22 na kushinda mataji 31 alisema hataweza kucheza dhidi ya Barcelona atakapoondoka klabuni hapo.


Iniesta maarufu kama ‘Magician’ ni mchezaji pekee kuwahi kuwa mchezaji bora (Man of the match) katika fainali ya EURO, fainali ya Kombe la Dunia na fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kiuongo huyo bora duniani anatarajiwa kwenda kukipiga China ambapo inadaiwa atalipwa mkwanja mara mbili ya ule anaolipwa Barcelona. Aidha, Iniesta amesema hataki tena kucheza Soka Bara la Ulaya kwa sababu atakutana katika mechi na timu yake iliyomlea Barcelona jambo ambalo anaona kwake haitakuwa vyema kupambana na mlezi wake.
WWW.EDUSPORTSTZ.COM

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment