Type something and hit enter

On


Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB), imewasihi wanafunzi wote ambao wanatarajia kutuma maombi ya kupatiwa mkopo watambue kwamba watakuwa na jukumu la kurejesha pindi watakapohitimu.


Akiongea na vyombo vya habari mapema leo Mei 10, 2018, wakati wa ufunguzi rasmi wa kuanza kutuma maombi ya mkopo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Abdu-Razaq Badru amesema kwamba mkopo ni lazima urejeshwe na kuongeza kuwa hakuna njia ambayo wanufaikaji wa mikopo wataweza kukwepa kulipa labda kwa wale ambao wamefariki.

"Huu ni mkopo na sio zawadi na mkopo unalipwa, siku unapoamua kuomba ukumbuke kwamba utalipa na bahati nzuri kwasasa utaratibu wa kulipa umeboreshwa, lakini unaposhindwa kulipa kwa hiari basi zipo namna nyingine nyingi za kukusaida kulipa na sasa tumezamilia kwa kila atakaekopa ni lazima alipe kwa namna yoyote ile labda akifariki dunia hatalipa", amesema Badru

Katika mwaka wa fedha 2018/2019 serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 427 kwaajili ya wanafunzi 122,000 wa elimu ya juu ambapo wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza 47,000 watanufaika, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya wanafunzi 7000 ukilinganisha na mwaka 2017.

Taaluma ambazo zitapewa kipaumbele katika kupata mkopo ni waombaji wa fani za Ualimu wa masomo ya sayansi, Sayansi ya afya na mwanadamu, Uhandisi, Kilimo, Usindikaji wa bidhaa na Usafirishaji.

Zoezi la kutuma maombi ya mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu limeanza leo Mei 10 na litafungwa rasmi Julai 15, 2018.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

Enter your email address:
Delivered by EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment