BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 31 May 2018

31 May

KAULI YA MWISHO YA KINANA KWA WANACCMAliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndg. Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa CCM kiujumla kumpa ushirikiano Katibu Mkuu mpya ambaye ni Dkt. Bashiru Ally kama walivyo kuwa wanampa yeye kipindi alipokuwa kwenye nafasi hiyo
31 May

MAKKA " SITAITUMIA JEZI NAMBA 8 KWA HESHIMA YA MCHEZAJI MPYA"kumekuwa na tetesi nyingi sana kuhusu usajili kujiandaa kwa msimu ujao wa ligi kuu tanzania bara.

Timu kubwa hasa simba, yanga, na azam zimekuwa zikihusishwa na wachezaji mbalimbali.

Klabu ya yanga imeonekana tofauti kidogo na misimu mingine katika mbinu za kufanya usajili kimya kimya bila ya tetesi zozote.

Jana kupitia ukurasa wa instagram wa klabu ya yanga ulitoa taarifa kwa kumtumia mchezaji makka edward na kutoa ujumbe ulisomeka ya kwamba hatatumia jezi namba 8 kwa msimu ujao kwa heshima ya mchezaji anaekuja.

Lakini klabu hiyo haikutoa taarifa rasmi ya nani atavaa jezi hiyo mpka pale utambulisho rasmi utakapofanywa.

pia kumekuwa na taarifa ya kwamba yanga wamemrudisha mchezaji wake wa zamani mrisho ngassa akitokea ndanda ambako alikuwa kwa msimu mmoja alipojiunga kutoka mbeya city.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
31 May

MAGAZETI YA LEO MAY 31 KWA TANZANIA NA ULAYAKama kawaida Edusportstz tayari imeshakusogezea stori kubwa zilizotengeneza headline katika kurasa za mbele na nyuma za Magazeti ya Tanzania Leo juma tano ya May 31/2018. Chukua time yako kwa kupitia Stori zote kali za udaku, siasa, michezo, burudani na mambo mengine mbali mbali.

Wednesday, 30 May 2018

30 May

SIMBA APELEKA KILIO KINGINE YANGA


Ikiwa timu za ligi kuu bara zikiwa zinajiandaa kwa msimu ujao kwa kufanya sajili mbalimbali.

Klabu ya simba tayari imeshawachukua wachezaji wawili ambapo mmoja ni adama salamba toka lipuli ambapo wiki kadhaa alihusishwa na mpango wa yanga kwenda kuisaidia katika michuano ya shirikisho Africa. lakini siku mbili nyuma mchezaji huyo alijiunga na simba.

Toka jana kumekuwa na tetesi ya kwamba  huenda PAPII TSHISHIMBI akajiunga na simba toka yanga baada ya kile kinachoelezwa kwamba huenda yanga na mchezaji huyo mkataba wake umevunjwa.

Simba anajiandaa na mashindano ya Champions ligi Afrika msimu ujao pengine ikawa ni sehem ya maandalizi hayo.

PAPII katika msimu wake wa kwanza Vpl amekuwa katika kiwango bora licha ya klabu yake kufanya vibaya pia amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa mpira wa miguu nchini kutokana na ubora huoEDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
30 May

MTU MZEE ZAIDI DUNIANI ATOA YA MOYONI KUHUSU KUVUTA TUMBAKU

'
Fredie Blom anasema kuwa hakuna siri kuhusu maisha yake marefu
Fredie Blom alihudumu wakati mwingi kama mfanyikazi katika shamba na katika sekta ya ujenzi nyakati za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini lakini huenda hivi karibuni akatambuliwa kuwa mtu mzee zaidi duniani , kama anavyoripoti mwandishi wa BBC Mohammed Allie kutoka Cape Town.


Ijapokuwa aliwacha kunywa pombe miaka mingi iliopita , Fredie Blom ni mvutaji sigara wa mara kwa mara.

''Kila siku mimi huvuta sigara mara mbili au tatu, mimi hutumia tumbaku yangu kwa sababu sivuti sigara za kawaida. Shinikizo ya kutaka kuvuta sigara ipo juu''.

''Mara nyengine mimi hujiambia nitawacha lakini naona kana kwamba najidanganya. Kifua changu kinanishinikiza kuvuta hivybasi hulazimika kutengeza kiko changu cha tumbaku.Namlaumu shetani kwa hayo kwa kuwa ana nguvu sana''.

Tanzania: Wamiliki wa blogu, TV na redio mtandaoni watakiwa kujisajili
Raheem Sterling akemewa kwa kuchora tatuu ya bunduki mguuni
Washukiwa wa ufujaji wa pesa Kenya wafikishwa kortini
Umaarufu wake
Kitu kimoja kinachokugusa moyoni unapokutana na mzee huyo ni vile alivyoimarika kiafya na hali yake. Akiwa mrefu na mwenye nguvu anatembea bila usaidizi wowote mbali na kwamba hana ugonjwa wowote.

Mfanyikazi huyo wa zamani wa shambani ambaye alifikisha umri wa miaka 114 mwezi Mei tarehe 8 anasemekana kuwa mtu mzee zaidi aliyehai ijapokuwa hilo halijathibitishwa na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness.

Taji hilo lilikuwa likishikiliwa na mwanamke wa Jamaica Violet Moss Brown hadi tarehe 15 Sepetmba 2017 wakati alipofariki akiwa na umri wa miaka 117.

Kitabu cha Guiness cha rekodi za dunia kinasema kuwa bado kinatafuta ushauri kutoka kwa wataalam wa historia kuthibitisha ni nani anayeshikiia taji hilo la mwanamke mzee zaidi pamoja na lile la mwanamume mzee zaidi.

Kulikuwa na wasiwasi kuhusu maisha yake hadi alipotoa kibali chake cha kuzaliwa
Bwana Blom, mwenye masharubu na ndevu za kijivu hana siri yoyote kuhusu maisha yake marefu.

''Kuna kitu kimoja -Ni Mungu aliye juu mbinguni. Sina chochote ninaweza kuanguka muda wowote, lakini Mungu ananizuilia ,ana nguvu zote''', alipoulizwa ni nini haswa kinachomfanya kuendelea kuishi.

Nahisi vyema kabisa , niko shwari .Moyo wangu una nguvu lakini ni miguu yangu pekee ambayo imeanza kukubali uzee wangu -siwezi kutembea tena vile nilivyokuwa nikitembea, anazungumza kwa lugha ya Afrikaaner kwa sauti ya juu.

Amejipatia umaarufu ambao umewafanya raia pamoja na maafisa wa serikali wakiwemo mawaziri kumtembelea nyumbani kwake huko Cap Town.

Amesema kuwa ni hisia nzuri kujua kwamba watu wanakuthamini.

Katika siku yake ya kuzaliwa , duka moja la jumla na idara ya maswala ya kijamii serikalini ilimpatia keki kubwa.

Alifanya kazi hadi miaka ya 80
Janetta, ambaye ni mkewe bwana Blom kwa miaka 48 ambaye ni mdogo wake kwa miaka 29 anasema kuwa mumewe amekuwa na afya njema na alienda hospitalini mara moja pekee - miaka mingi iliopita wakati alipokuwa na tatizo la goti.

Anasema kuwa watu wengi awali walikuwa na wasiwasi kuhusu umri wa mumewe.

Kulikuwa na maswali kuhusu swala hilo wakati alipotuma ombi la kupata kitambulisho miaka kadhaa iliopita , lakini mpwa wake alienda mjini London ili kupata cheti chake cha kuzaliwa ambacho kilitoa thibitisho lililohitajika.

Sihle Ngobese , msemaji wa idara ya West Cape kuhusu muendelezo wa kijamii aliniambia kwamba ukweli kwamba serikali ilimpatia bwana Blom kitambulisho kilichorekodi siku yake ya kuzaliwa kuwa tarehe 8 mwezi Mei 1904 ni dhihirisho tosha.

Blom anakumbuka ujana wake akijaribu kuwinda ndege kwa kutumia manati
Alikuwa mdogo wakati bwana Blom alipoondoka Adelaide, mji mdogo mashariki mwa Cape Town kuelekea Cape Town.

Kwa kuwa hakuhudhuria masomo shuleni hawezi kusoma wala kuandika.

Badala yake macho yake hujifunga funga wakati anapofikiria ujana wake.

"Wakati nilipoamka alfajiri nilipenda kwenda nje na kuuangalia ulimwengu. Mara nyengine ningechukua manati yangu na kuwapiga ndege -nilihisi vyema wakati nilipoangalia ukanda wangu na ulikuwa umejaa ndege ambao nilikuwa nimewapiga.Mkewe aliniambia kwamba hali chochote maalum. Hupendelea kula nyama katika kila chakula lakini pia hula mboga nyingi.

Bwana Blom bado ana nguvu za kuosha nguo na kuvaa ijapouwa kulingana na mkewe hupata shida kuvaa viatu vyake. Mara nyengine hupendelea usaidizi wa mjukuu wake.

Kwa mtu ambaye alianza siku yake saa kumi na nusu alfajiri katika kipindi alichokuwa akifanya kazi , bwana Blom huamka kuchelewa na hafayi mambo mengi nyumbani.

''Siwezi kufanya chochote -siwezi hata kupanda ngazi tena . Mimi huketi tu. Sina muda na upuzi uliopo kwenye runinga''.

Anapendelea sana kuketi nje ya nyumba yake na kuvuta sigara

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
30 May

IJUE HATMA YA WATANZANIA 11 WALOSHITAKIWA KWA UBAKAJI AFRIKA KUSINI

Vijana wa Tanzania

Vijana 11 raia wa Tanzania waishio Johannesburg, Afrika Kusini walioshtakiwa kosa la ubakaji wameachiliwa huru na hakimu mkazi wa Mahakama ya Johannesburg.

Walikuwa wameshtakiwa kwa makosa ya kumteka nyara na kumbaka mwanamke mjamzito Thelma Mondowa raia wa Zimbabwe mwaka uliopita.

Waliachiliwa huru na Jaji Metisie kwa kukosekana kwa ushahidi.

Wakili wa upande wa mashtaka wa serikali alikuwa amemfahamisha hakimu kuwa Bi Thelma Mondowa aliamua kurejea Zimbabwe na wameshindwa kupata anwani yake.

Mwanamke huyo iliarifiwa alikuwa akitoka kazini na mfanyakazi mwenzake wa kiume pale ghafla walipovamiwa na kundi la wanaume wenye silaha na wakamvuta mwanamke huyo kabla ya kumpiga mfanyakazi mwenzake ambae baadaye alifanikiwa kutoroka.

Kisa hicho kilitokea mnamo 15 Mei mwaka 2015 katika barabara ya 270 Lilian Ngoyi mjini Johannesburg.

Baada ya mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu polisi na wakafanikiwa kufika eneo la tukio na kuwakuta wanaume hao wakimbaka kwa zamu mwanamke huyo.

Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo ambapo tukio lilidaiwa kufanyika na kumuokoa mwanamke huyo na kumpeleka hospitalini.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
30 May

FAIDA 10 MUHIMU KWA AFYA YAKO ZITOKANAZO NA MAFUTA YA NAZI

Mafuta ya nazi 

FAIDA KUMI MUHIMU KWA AFYA YAKO ZITOKANAZO NA MAFUTA YA NAZI

1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo:

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.

2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula:

Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.

3. Mafuta ya nazi hung’arisha ngozi:

Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.

4. Huongeza nguvu mwilini:

Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’ ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.

5. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya:

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

6. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama:

Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.

7. Huzuia maradhi mengi hatari mwilini:

Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid. Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mine na utaona maajabu.

8. Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu:

Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

9. Hutumika kulainisha uke mkavu:

Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.

10. Husaidia katika ugonjwa wa mzio/aleji:

Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza, moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.

MHIMU: Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ
30 May

MAGAZETI YA SIASA,MICHEZO NA BURUDANI LEO MAY 30,2018
Kama kawaida Edusportstz tayari imeshakusogezea stori kubwa zilizotengeneza headline katika kurasa za mbele na nyuma za Magazeti ya Tanzania Leo jumanne May 302018. Chukua time yako kwa kupitia Stori zote kali za udaku, siasa, michezo, burudani na mambo mengine mbali mbali.

Tuesday, 29 May 2018

29 May

HESHIMA YA RAIS WA MISRI KWA MO SALAH

mo salah

Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi alithibitisha kuwa aliwasiliana na Mohamed Salah kumtaka nyota wa Liverpool kupona haraka kutokana na kuumia.

Salah, mwenye umri wa miaka 25, aliumia jeraha la bega wakati upande wake ulipoteza 3-1 kwa Real Madrid katika fainali wa Ligi ya Mabingwa Jumamosi.

Kulikuwa na hofu za awali Salah asingecheza Kombe la Dunia, lakini nyota huyo wa kimataifa wa Misri anajiamini kuwa atakuwa vizuri kwa mashindano hayo.

El-Sisi alithibitisha Salah alipendekeza kuwa atakuwa tayari kwenye tukio  la kuhamasisha amani  nchini Urusi, ambapo Misri itawakabili Saudi Arabia na Uruguay katika Kundi A.

"Nimewasiliana na mtoto mzuri wa Misri na mwanangu, Mohamed Salah, ili kumhakikishia baada ya kuumia kwake," aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Kama nilivyotarajia, nimemwona shujaa ambaye ni mwenye nguvu kaumia na amefurahi kuendelea na  mashindano ."

Aliongeza: "Nilimwambia kuwa wewe ni icon ya Misri, na mwenye heshima kubwa.
"Ninamwombea Mwenyezi Mungu, kama baba kwa mwanawe, kwa ajili ya kupona haraka sana."

Misri wataanza kampeni yao ya Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay Juni 15.