RIDHIWANI KIKWETE ATOA YA MOYONI JUU YA MAUAJI YA MDOGO WAKE JONH HECHE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 28 April 2018

RIDHIWANI KIKWETE ATOA YA MOYONI JUU YA MAUAJI YA MDOGO WAKE JONH HECHE


Mbunge wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh. Ridhiwani Kikwete amefunguka na kusema kitendo cha polisi mwenye namba E1156 Koplo William Marwa ambaye anadaiwa kufanya mauaji kwa mdogo wa Heche kimemsikitisha sana. 

Ridhiwani amefunguka hayo baada ya Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Tarime na Rorya kudai kuwa linamshikilia polisi huyo kwa tuhuma za kumchoma kisu Bwana Chacha Heche Suguta ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche.

"Kitendo kilichotokea sio tu kimesikitisha ukoo wa Bwana Heche lakini kwangu binafsi. Jeshi letu limetengenezwa kulinda watu na mali zao sio kuumiza wasio na hatia. Ni imani yangu Serikali itasimamia haki kwa familia ya Heche. Poleni sana kwa msiba. Mungu awape subira John Heche" alisema Ridhiwani 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe amethibitisha kumshikilia askari wake mwenye namba E1156 Koplo William Marwa kwa tuhuma za kusababisha kifo cha kijana Suguta Chacha mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Sirari wilayani Tarime mkoani Mara kwa kumchoma Kisu.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ