RAIS JPM AIPANDISHA HADHI MANISPAA YA DODOMA KUWA JIJI RASMI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Thursday, 26 April 2018

RAIS JPM AIPANDISHA HADHI MANISPAA YA DODOMA KUWA JIJI RASMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 26, 2018 ameupandisha hadhi mji wa Dodoma na kuwa jiji, huku akimtaja Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wa sasa kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo jipya.


Kufatia sherehe hizo za muungano, katika viwanja vya Jamhuri vilivyopo Dodoma ambapo ndipo zilipofanyikia sherehe za miaka 54 ya Muungano kitaifa, Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo la kuipandisha hadhi manispaa ya Dodoma ambayo pia ilikua makao makuu ya serikali kuwa jiji jipya. 
Pia amesisitiza kuwa "Azma ya serikali kuhamia Dodoma ipo pale pale hakuna kurudi nyuma na tayari zaidi ya watumishi 3800 wameshahamia na mimi kama nilivyo ahidi mwaka huu nahamia Dodoma. Dodoma ndio makao makuu kwa hiyo kuanzia leo kwa mamlaka mliyonipa watanzania Dodoma ni Jiji", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "kwa hiyo maandalizi yote ya kisheria yaanze kutumika katika jiji hili jipya na hili litakuwa Jiji la pekee yake kwasababu lipo kati ya Tanzania".

Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli amewahakikishia wananchi wa Tanzania kuwa wako safi bila ya kujali vyama vyao.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:
Delivered by EDUSPORTSTZ