Type something and hit enter

On

Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako, amesema anaitumia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kama changamoto na chachu ya kuendelea kufanya kazi nzuri.

Ndalicho ameyasema hayo Jana Aprili 17 wakati akijibu hoja za ripoti ya CAG iliyosomwa wiki iliyopita bungeni.

Wiki iliyopita mawaziri wanane walifanya mkutano na waandishi wa habari wakijibu hoja za ripoti ya CAG.

“Serikali ya awamu ya tano kwenye suala la udhibiti haina utani kila mtu ameona kazi ambayo imefanyika, tunapopata ripoti ya CAG, inatupa chachu ya kuendeleza na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano,” amesema

Amesema kama CAG alivyoshauri, watafanyia kazi mapendekezo ya CAG na pia watawachukulia hatua watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma.

Ndalichako alizungumzia hoja ya CAG kuhusu ukusanyaji hafifu wa fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na akasema, tangu serikali ya awamo ya tano iingie madarakani, kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa madeni hayo.

“Taarifa ya CAG 2015/16 hadi 2016/17 inaionyesha kuwa makusanyo yameongezeka kutoka Sh28bilioni hadi Sh 116bilioni. Hilo ni ongezeko la asilimia 300. Takwimu hazidanganyi,” amesema

Hata hivyo amesema bado makusanyo hayo hayatoshelezi na ameitaka Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kuhakikisha ukusanyaji wa mikopo unaimarishwa.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment