JPM KUZINDUA UKUTA WA TANZANITE LEO: SOMA KUJUA UJENZI WA UKUTA HUO - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 6 April 2018

JPM KUZINDUA UKUTA WA TANZANITE LEO: SOMA KUJUA UJENZI WA UKUTA HUO

Rais Magufuli aliagiza kujengwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite mwaka jana

Rais John Magufuli wa Tanzania, leo anatarajiwa kuzindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite,iliopo eneo la Mererani, kaskazini mwa nchini Tanzania
Sehemu ya ukuta huo

Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umejengwa kufuatia agizo lililotolewa na Rais John Magufuli, kama jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.

Awali, Mwezi Februari, wakuu wa vyombo vya usalama, walitembelea eneo hilo, kuukagua ukuta huo uliojengwa kwa gharama za Kitanzania isiyozidi bilioni 6.

Walisisitiza kuwa lengo la kujengwa kwake ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.
"Waanze kujenga ukuta eneo hilo lote na kazi hii ifanyike haraka, watakapojenga ukuta wataweka kamera na patakuwa na mlango mmoja ambapo patajengwa vifaa maalum, nataka niwaeleze ukweli ndugu zangu wa Simanjiro hata kama utameza Tanzanite itaonekana" Agizo la Rais Magufuli mwaka uliopita

Wakitoa taarifa kwa viongozi wa ulinzi, wataalamu waliojenga ukuta huo, walisema licha ya kufanikisha ujenzi huo, changamoto mbalimbali walikutana nazo ikiwemo hatari inayo ukabili ukuta huo, kutokana na wachimbaji kulipua baruti, karibu na ukuta, hivyo kusababisha hatari za kuharibika haraka.

Ugumu wengine walioupata ni uchimbaji katika maeneo yenye miamba.

Chanzo: BBS
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

1 comment: