TSHISHIMBI ATWAA UCHEZAJI BORA FEBRUARY - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Tuesday, 13 March 2018

TSHISHIMBI ATWAA UCHEZAJI BORA FEBRUARY

Mchezaji wa yanga Tshishimbi aliyechaguliwa kuwamchezaji bora wa mwezi february

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limemtangaza Mchezaji, Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Februari.

Tshishimbi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kuvuna alama 12 huku akifunga mabao matatu na akitengeneza moja.

Mechi ambazo Tshishimbi alihusika kwenye ushindi katika mwezi Februari ni dhidi ya Majimaji, Njombe Mji, Ndanda na Lipuli ya Iringa.

Pius Buswita (Young African) na Emmanuel Okwi (Simba SC) ni wachezaji ambao waliokuwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo kwa mwezi huu wa pili.

Tshishimbi ambaye ni mshindi wa tuzo hii, atazawadiwa kitita cha milioni moja sambamba na king'amuzi cha Azam TV.EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ