RAIS JPM AGUSWA NA MSIBA WA ALIYEKUWA MBUNGE WA KIGOMA MJINI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Wednesday, 7 March 2018

RAIS JPM AGUSWA NA MSIBA WA ALIYEKUWA MBUNGE WA KIGOMA MJINI

Rais Wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania

Leo March 7, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kufuatia kifo cha Dkt. Walid Amani Kaburu.

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Dkt. Walid Amani Kaburu kilichotokea usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili DSM alikokuwa akipatiwa matibabu.” -Rais Magufuli

“Dkt. Walid Amani Kaburu atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, na alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.” -Rais Magufuli

“Natoa pole kwa familia yake, wana CCM wote, wananchi wa Kigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu” -Rais Magufuli
Marhemu Dr Amani Kaburu

Pamoja na salamu hizo Rais Magufuli ameiombea familia ya Marehemu na wote walioguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi na amemuombea Marehemu apumzike mahali pema peponi, Amina.