NAIBU WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAKAZI ASHUTUSWA NYUMBA ZILIZOJENGWA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 5 March 2018

NAIBU WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAKAZI ASHUTUSWA NYUMBA ZILIZOJENGWA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amebaini uwepo ya nyumba za watanzania zilizojengwa katikati ya mpaka wa Tanzania na Kenya huku eneo moja la nyumba hizo likiwa upande wa Kenya.

Katika ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro mkoa wa Tanga mhe Mabula alijionea jinsi nyumba zilivyojengwa bila utaratibu wa kuacha umbali wa mita mia kama eneo huru.

Eneo lililoathirika zaidi na ujenzi huo, ni katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga ambapo asilimia kubwa ya wakazi wake wamejenga nyumba zao zikiwa karibu kabisa na mpaka huku baadhi yake sehemu ikiwa upande wa Tanzania na nyingine upande wa Kenya.

Hata hivyo, Naibu Wzairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameshuhudia upande wa Tanzania katika eneo la Horohoro ukiwa umezingatia umbali unaotakiwa kati ya mpaka ukilinganisha na wakenya wanaoishi kijiji cha Jua kali Lungalunga ambao wamejenga karibu kabisa na mpaka wa Tanzania.

Kufuatia hali hiyo kuna uwezekano mkubwa wakazi wanaoishi katika maeneo hayo ya mpakani kukumbwa na zoezi la kubomolewa nyumba zao ingawa kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea baina ya Tanzania na Kenya kuhusu umbali gani pande hizo zinaweza kukubaliana ili kunusuru baadhi ya wananchi wa pande zote mbili.


  EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ