MWENYEKITI WA MATANDAO WA WANAFUNZI APOTEA KUSIKOJULIKANA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Wednesday, 7 March 2018

MWENYEKITI WA MATANDAO WA WANAFUNZI APOTEA KUSIKOJULIKANA


Mwenyekiti Wa mtandao Wa wanafunzi

TAARIFA zilizoenea mchana huu zinadai kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajulikani alipo tangu jana saa sita usiku.

Marafiki za Nondo wamedai alituma ujumbe kwa viongozi wenzake wa TSNP kuwa yuko katika hatari na baada ya kutuma ujumbe huo simu yake ilikuwa ikipokelewa lakini hakuwa akiongea chochote, na baada ya muda alianza kujiondoa kwenye magroup ya WhatsApp.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Mtandao wa Wanafunzi, kuhusu Abdul ni kweli hajulikani yuko wapi mpaka sasa, hata Wazazi wake(Mama na Baba yake mdogo) hawajui yuko wapi. Viongozi wa Mtandao wa Wanafunzi wamefika Kituo cha Polisi kilichopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwaajili ya kutoa taarifa za kupotea kwake
Feb 18, 2018, Nondo alijitokeza na kuikosoa mienendo ya Jeshi la Polisi na Waziri wa Mambo ya Ndani, na mara ya mwisho kuongea na wanahabari, alishinikiza Waziri Mwigulu Nchemba ajiuzulu. Hivi karibuni pia akizungumza na wanahabari aliwataka TAHLISO waache kuwa wasemaji wa wizara na serikali na kuwataka wakumbuke majukumu yao mazito ya kusemea wanafunzi wa vyuo vikuu kwa sababu wanalipishwa ada vyuo vikuu.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ