MPANGO WA TRUMP WA KUTOZA USHURU BIDHAA YA CHUMA WA PASUA VICHWA WAFANYABIASHARA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 2 March 2018

MPANGO WA TRUMP WA KUTOZA USHURU BIDHAA YA CHUMA WA PASUA VICHWA WAFANYABIASHARA


Viwanda vya chuma vya Ulaya kama hii nchini Ujerumani zaweza athirika vibara ya ushuru European steel factories, like this one in Germany, could be hit by the US tariffs

Washirika wakubwa wa biashara wa Marekani wamekasirishwa na tangazo la Rais wa nchi hiyo Donald Trump juu ya mpango wa kutoza ushuru kwa bidhaa za chuma na aluminiam zinazoingizwa.

Umoja wa Ulaya na Canada kwa pamoja zimesema zitafanyia kazi uamuzi huo, kupingana na tamko hilo.

Rais wa Tume ya Ulaya Jean Claude Juncker amesema uamuzi huo wa Marekani wa kutoza ushuru utahatarisha maelfu ya kazi barani Ulaya.

Nchi za Mexico, China na Brazil wanasema wataziangaliz hatua za kulipiza kisasi.

Bw Trump aliweka ujumbe katika akaunti yake ya Twitter na kusema Marekani ilikuwa imekumbwa na "sera mbovu na zisizo sawa za biashara".

Alisema bidhaa za chuma zinazo ingizwa zingetozwa ushuru ya asilimia 25 na aliminiam asilimia 10.

Lakini wakosoaji wake wamesema ushuru hizi hazitafanikiwa kulinda ajira za Marekani na hatinaye zingepandisha bei za bidhaa kwa wanunuzi.

Habari ziliathiri hisa za Asia ambazo zilishuka siku ya Ijumaa, huku hisa ya Japan, Nikkei ikipoteza zaidi ya asilimia 2.

Hisa za kampuni kubwa ya magari ya Japan, Toyota zilishuka na zaidi ya asilimia 2 na hisa za Nippon Steel pia zilishuka kwa zaidi ya asilimia 4.

Toyota imesema maamuzi ya Marekani " yangeathiri sana watengeneza magari na wanunuzi"
Marekani inategemea uingizaji chuma kutoka nchi zaidi ya 100
Trump amesema nini?

Bw Trump ameahidi kuijenga tena sekta ya chuma na aluminiam nchini humo ambayo amesema imetendewa vibaya na nchi nyingine hasa China kwa miongo mingi.

"Kama nchi yako haiwezi kutengeza aluminiam na chuma..ni kama hauna nchi tena," alisema

"Tunahitaji watengenezaji wazuri wa aluminiam ili kujilinda"

Tangu aingie madarakani amekuwa akisema kuwa uingizaji wa bidhaa kutoka China imedhoofisha viwanda.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
WEKA EMAIL YAKO KUTUMIWA HABARI


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment