MAZUNGUMOZO YA TRUMP NA RAIS WA KOREA KUSINI KUELEKEA MJUTANO WAKE NA KIM JONG UN - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 17 March 2018

MAZUNGUMOZO YA TRUMP NA RAIS WA KOREA KUSINI KUELEKEA MJUTANO WAKE NA KIM JONG UNRais wa Marekani Donald Trump amezungumza na rais wa Korea Kusini Moon Jae In kuhusu mkutano wake na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Viongozi hao wawili katika mazungumzo hayo wamesisitiza kuwa endapo Korea Kaskazini itachagua njia iliyo sahihi basi kutakuwa na mustakabali mzuri kwa taifa hilo.

Kwa mujibu wa habari,Trump na Moon wanaamini kuwa vitendo na sio maneno ndio vinavyohitajika kusuluhisha masuala ya Korea Kaskazini na majaribio yake ya makombora ya nyuklia.

Endapo mkutano huo utafanyika utakuwa ni wa kwanza kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini na rais wa sasa wa Marekani.

Mkutano unatarajia kufanyika mwisho wa mwezi MeiEDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ