BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 31 March 2018

31 March

Vyakula Vinavyoongeza Nguvu Za Kiume Mwilini


Vyakula Vinavyoongeza Nguvu Za Kiume Mwilini
Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. 
Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.


Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.


Sababu za kukosa nguvu za kiume
Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.


1. Blueberry

Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume.


Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.


3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.


Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.


4. Karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.


5. Vitunguu saumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.


6. Ndizi
Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).
7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.


Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.


Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.


Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.

NINI MAONI YAKO? ACHA UJUMBE WAKO HAPA CHINI!!!

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
31 March

YAFAHAMU MAJENGO 10 MAREFU ZAIDI BARANI AFRIKA

Mara nyingi wabunifu mbalimbali wamajengo wamekuwa wakileta style mbalimbali za majengo yanayoendana geografia ya sehemu husika,gharama na ukuaji wa teknolojia dunian.Leo Edusportstz inakuletea list ya majengo kumi marefu zaidi Africa.
31 March

ZIJUE MARUFUKU ZA RAIS JPM TANGU ALIPOINGIA MADARAKANI MPAKA SASA

Rais wa Tanzania John Magufuli

Rais wa Tanzania,John Magufuli ameonekana kuwa ni kiongozi anayetoa maamuzi ya haraka kwa kutoa marufuku ya jambo au kuwaachisha kazi watendaji katika nyadhifa zao.

"Kutumbua majipu" ni neno ambalo limekuwa maarufu katika vinywa vya wengi baada ya kiongozi huyo kuwafukuza kazi watendaji pale ambapo anaona mambo hayaendi sawa.

Mfano hivi karibuni, Rais Magufuli amewaachisha kazi wakurugenzi wawili mkoani Kigoma mara tu baada ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kumkabidhi ripoti ambayo ilikuwa na matokeo mabaya katika eneo hilo.

Lakini haya chini ni orodha ya marufuku aliyoyatoa Rais Magufuli yanaoathiri sekta mbali za serikali ya Tanzania tangu aingia madarakani;
Polisi wamekuwa wakitahadharisha juu ya maandamano mara kwa mara

Maandamano na mikutano ya Kisiasa
Rais Magufuli amenukuliwa akisema shughuli za siasa ikiwa ni pamoja na maandamano na mikutano ya hadhara isimame hadi uchaguzi ujao mwaka 2020.

Amedai baada ya uchaguzi uliopita, "sasa ni wakati wa kazi tu"

Vyombo vya usalama vimekuwa vikitahadharisha mara kwa mara kuwa hawatasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hilo.

Aidha maafisa hao wamewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi na badala yake kuwasihi waendelee kushirikiana katika kujenga Umoja wa taifa la Tanzania.

Hata hivyo, maafisa hao kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya habari wamebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.

Shughuli za siasa, ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ni haki ya raia kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.
Rais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini alipofanya ziara ya kushtukiza Machi 2017

Usafirishwaji wa madini nje ya nchi

Mwaka jana, Rais Magufuli alipiga marufuku usafirishwaji wa madini yasiyo chenjuliwa mpaka pale kodi za nyuma ziwe zimelipwa.

Serikali hiyo iliweka mpango wa utaratibu utakaowezesha ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia yaani Smelter, hapa nchini ili kudhibiti upotevu wa mapato na kutengeneza mapato kwa watanzania.
Wanafunzi watakaopata ujauzito wakiwa shuleni hawataruhusiwa tena kurudi shuleni

Waliopata mimba shuleni wasirejee shule
Rais Magufuli alisema kuwa chini ya uongozi wake wanafunzi wa kike ambao watakaopata ujauzito wakiwa shuleni hawataruhusiwa tena kurudi shuleni.

Aidha Magufuli alikumbusha kwamba sheria inasema mwanaume ambaye atapatikana na hatia ya kumpa mimba mtoto wa shule, atafungwa jela miaka 30.

Magufuli aliongeza kwamba mwanaume huyo atapata fursa ya kutumia nguvu alizotumia kumpachika mimba msichana huyo, kufanya kilimo akiwa gerezani.

Nchini Tanzania kuna takriban wasichana 8,000 ambao huacha shule kila mwaka kutokana na kuwa wajawazito, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Human Rights Watch.
Miongoni mwa meli za kigeni zilizosajiliwa Tanzania

Usajili wa meli mpya
Miongoni mwa mambo ambayo yamepigwa marufuku nchini Tanzania tangu rais Magufuli aingie madarakani ni pamoja na kusitisha usajili wa meli mpya nchini humo 'mpaka itakapotangazwa vinginevyo'.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli aliagiza utoaji wa vibali na usajili usimame hadi hapo uchunguzi kina ufanyike kwa meli zote 470 ambazo zimesajiliwa Tanzania na zinapeperusha bendera ya Tanzania.

Agizo hilo lilikuja baada ya taarifa za kukamatwa kwa meli zilizokuwa zimepakia shehena za dawa za kulevya na silaha huku zikiwa zinapeperusha bendera ya Tanzania.

Mbali na marufuku hizo ambazo zimetolewa na yeye mwenyewe zipo nyingine ambazo zimetajwa wakati wa utawala wake.
shisha

Uvutaji wa shisha ni marufuku Tanzania

Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa shisha nchini humo na kulitaka jeshi la polisi kufanya kila juhudi kutokomeza uraibu huo.
Katazo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bwana Paulo makonda lilifuatiwa na lile la Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambapo alitoa agizo na kusema uvutaji shisha umekuwa ukichangia katika kudorora kwa maadili miongoni mwa vijana, na kuwapunguzia uwezo wa kiakili na kimwili wa kufanya kazi.
Kenya wakiteketeza pombe haramu 2015

Viroba
Mapema mwaka jana,pombe zilizokuwa zinauzwa kwenye mifuko midogo ya plastiki zimepigwa marufuku kuuzwa katika maeneo yeyote nchini humo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Friday, 30 March 2018

30 March

TETESI ZA SOKA BARANI URAYA LEO

Manchester City inatuma kusaini makataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid Mhispania Isco

Manchester City wanaamini wanaweza kusaini makataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid Mhispania Isco msimu huu wa majira ya joto. Mkataba kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 unaweza kuwa wa thamani ya Euro milioni 75. (Mirror)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ubelgiji Mousa Dembele, mwenye umri wa miaka 30, hatasaini makataba mpya na Tottenham kabla ya Kombe la Dunia la mwaka huu, na hivyo kuibua maswali kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo. (Telegraph).

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29, atawasilisha maombi yake ya kutaka kuhamia Real Madrid msimu huu wa majira ya joto. Mchezaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 25 na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Alvaro Morata ni mmoja wa washambuliaji ambao Bayern Munich inamtaka kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Pole iwapo watampoteza. (AS - in Spanish)

Winga wa Crystal Palace Andros Townsend anasema kuwasaidia Eagles kuepuka kushuka daraja ni suala analolipa kipaumbele zaidi.

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Paris St-Germain midfielder Hatem Ben Arfa ametangaza kuwa ataondoka katika Ligi kuu ya Ufaransa mwisho wa msimu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, raia wa Ufaransa, amekuwa na uhusiano na Leicester City. (Sun).

Meneja wa Watford Javi Gracia amemkosoa Abdoulaye Doucoure, mwenye umri wa miaka 25, kwa kukataa kuhama katika msimu huu wa majira ya joto, huku Manchester United Tottenham, Liverpool na Arsenal kwa pamoja wakimthamanisha mchezaji huyo wa kiungo cha kati kwa kiwango cha Euro milioni 40. (Mail)

Mike Ashley ataanza mkakati wake wa kuuza klabu hiyo

West Ham wana imani ya kusaini mkataba na nahodha wa timu ya Urusi Fyodor Smolov. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, anayechezea klabu yake ya soka ya Krasnodar, anaweza kuhama kwa malipo ya Euro milioni £15m. (Mirror)

Mmiliki wa Newcastle United Mike Ashley ataanza mkakati wake wa kuuza klabu hiyo mara tu watakapohakikishiwa kwamba watafanikiwa kusalia Ligi ya Premia. (Telegraph)

Ligi ya Premia inatarajia kuanza kujaribu kupunguza idadi ya waamuzi katika mchakato wa video ya usaidizi wa maamuzi ya marefarii (VAR), badala ya kutegemea video rasmi bila kumuhusisha mtu yeyote. (Times)

Kijana Rhian Brewster mchezaji wa timu ya England ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 anasakwa na timu za Ligi ya Primia na nyingine

Manchester United imeanzisha msimu wa kupunguza gharama za tiketi za kuangalia michezo yake kwa vijana wenye umri wa miaka 16 hadi 25 kwa lengo la kuboresha uwepo wa watazamaji katika Old Trafford. (Telegraph).

Liverpool itaanzisha mazungumzo na kijana wa kikosi cha England kilichochukua kombe la dunia la vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Rhian Brewster. Klabu mbali mbali za Ligi ya Primia na nyingine zimeonyesha nia ya kumtaka na mkataba wake wa sasa unamalizika katika msimu wa majira ya joto. (Sun)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekosolewa na daktari wa zamani wa Bayern Munich, ambaye anasema kuwa anaweka mbele mafanikio mbele zaidi ya afya ya wachezaji. (Mail)

Winga wa Crystal Palace Andros Townsend anasema kuwasaidia Eagles kuepuka kushuka daraja ni suala analolipa kipaumbele zaidi.

Meneja wa timu ya Ubelgiji Roberto Martinez amemuonya mchezaji wa safu ya ulinzi ya Tottenham Toby Alderweireld mwenye umri wa miaka 29, kwamba nafasi yake katika kikosi cha Kombe la dunia imo mashakani ataendelea kutopendelewa na Mauricio Pochettino. (Guardian)

Winga wa Crystal Palace Andros Townsend, mwenye umri wa miaka 26, anasema kwamba licha ya kwamba ananuia kurejeshwa na England , kuwasaidia Eagles kuepuka kushuka daraja ni suala analolipa kipaumbele zaidi. (Mirror)

Meneja wa Cardiff City Neil Warnock amejipapatia jina la mtu wenye roho nyepesi, akiongeza kuwa: "Ninalia sana ninapotazama kipindi cha televisheni cha - I watch Call the Midwife." (Mail)

Lee Bowyer anasema alikuwa mshindani sana kama mchezaji wakati fulani lakini anataka sana kujulikana kama meneja anayewajali wachezaji Charlton. (Express)

Mchezaji wa safu ya kati wa Arsenal mfaransa Laurent Koscielny, mwenye umri wa miaka 31, ameanza kufanya yoga kwa ajili ya kurefusha muda wake kama mchezaji wa kulipwa. (Sun).

Chanzo: BBC swahili
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
30 March

THAMANI YA MSUVU KUPANDA KUFIKIA BIL 1.3 "MSUVA" AFUNGUKA HAYA

Kiungo mshambuliji wa timu ya Diffaa Al Jadi­da ya nchini Morocco, Simon Msuva (katikati).

SIMON Msuva ni kiungo mshambuliji wa timu ya Diffaa Al Jadi­da ya nchini Morocco ambaye ametua katika klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga.

Msuva ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Kitanzania wanaowakilisha nchi nje ya nchi wakicheza soka la kulipwa ambapo ameonyesha uwezo wa hali ya juu katika katika klabu yake hiyo kutokana na ubora wake katika kuzoea mazin­gira mapema na kuwa mfungaji mzuri.

Alijiunga na Al Jadida, Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000 ambalo ni zaidi Sh milioni 337 akitokea Yanga la­kini kwa sasa Waarabu wamemthamin­isha kwa euro 475,000, sawa na zaidi ya Sh bilioni 1.3.Moja ya mikakati yake ni kuona anafanikiwa kusonga mbele zaidi ili aweze kumfikia Mtanzania mwen­zake, Mbwana Samatta anayekipiga katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Championi Ijumaa imefanya mazun­gumzo na kiungo huyo ambaye ameelezea mikakati yake pamoja na kupanda kwa tha­mani yake kwa sasa.

Mazungumzo hayo ilikuwa ni baada ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya DR Congo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Msuva alipata nafasi ya kucheza na kuonye­sha uwezo mzuri.UNAZUNGUMZIAJE MCHEZO DHIDI YA DRC?

“Tunashukuru Mungu kwa matokeo tuliyoya­pata, tumepoteza mchezo wetu dhidi ya Alge­ria lakini kuna kitu fulani tumejifunza kutoka kwao, tukicheza mechi nyingi inatusaidia ku­tuweka vizuri.“DRC Congo wana timu nzuri ukiangalia mchezaji mmoja mmoja ni tofauti na tulivyo sisi lakini katika mpira lolote linaweza kuto­kea.

“Mpira unachezeka uwanjani na matokeo yanapatikana uwanjani, tulihamasishana wenyewe kwa wenyewe tuweze kuonyesha kitu na kweli tumefanikiwa kuonyesha kile ambacho Watanzania wanakihitaji.

“Tuliingia uwanjani kama timu, ma­kocha walituhamasisha, manahodha pamoja na wachezaji kwa ujumla tu­lijipanga ili kuhakikisha tunafanikiwa kufanya vyema na kweli matunda yam­eonekana kwa kupata ushindi.

UNAZUNGUMZIAJE SAPOTI YA MASHABIKI?

“Naomba mashabiki waiamini timu yao, shabiki kazi yake ni kushangilia timu yake, watambue kwamba timu ni hiihii hakuna tofauti, naamini tutafanya vizuri, waendelee kutupa sapoti ili tu­fanye vyema, wenzetu nje mashabiki wanashangilia timu yao hata wakifun­gwa.

KUCHEZA LIGI YA MABINGWA UKIWA NA TIMU YA MOROCCO, INA MAANA GANI KWAKO?

“Ni furaha kwangu, ni mara yangu ya kwanza kucheza mashindano hayo ni­kiwa Morocco, ninafanya kazi na timu yangu kwa kushirikina na wenzangu, nahitaji kupita njia ya Samatta ili nipate mafanikio makubwa.

UNA MABAO MANGAPI HADI SASA?

“Katika Ligi ya Mabingwa nina mabao manne katika Ligi Kuu ya Morocco nina sita, siyo mwendo mbaya kwangu.

MOROCCO WANAMCHUKULIAJE MSUVA?

“Wamenieleza kuwa mimi ndiyo Mtanzania wa kwanza kuonyesha kiwango kizuri kama changu katika ligi yao, nimefika na kuonyesha mabadiliko ya haraka ndani ya muda mfupi, wananikubali sana. Nimekopi vitu vyao mapema kutokana na kujitambua.

KIPI KILIKUFANYA UZOEE MAPEMA?

“Ligi yao haina tofauti sana na ligi ya Bongo kikubwa ni ushindani tu, niweweza kukutana na watu wanaojua mpira na ndiyo maana nimebadilika kwa haraka, mwalimu ameni­tengeneza na kunibadilisha, nimekuwa na uwezo mzuri wa kucheza katikati na hata mechi ya Stars na Congo nimecheza kati.

UNAZUNGUMZIAJE KUPANDA THA­MANI YAKO?

“(Kumbuka thamani yake ya dau la usajili im­epanda na sasa ni Sh bilioni 1.3) Namshukuru Mungu kuona thamani yangu inaendelea kupanda siku hadi siku, kikubwa ninamshuku­ru Mungu na kila kitu kinawezekana kupitia yeye, nitaendelea kupambana ili nisonge mbele.”


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
30 March

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU ASKARI WALIOHUSIKA NA KIFO CHA AKWILINA

Mwanafunzi wa NIT Akwilina aliyeuawa kwa risasi mapema mwaka huu. 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijni Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ameelezea hatua inayoendelea kuchukuliwa juu ya askari polisi sita waliokuwa wameshikiliwa kutokana na kifo cha mwanafunzi wa NIT Akwilina Akwilin, aliyeuawa kwa risasi mapema mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kamanda Mambosasa amesema polisi hao bado wapo kwenye uchunguzi kubaini ni nani anahusika, kwani mpaka sasa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuweza kumbaini.

“Wale walipokamatwa tulieleza bayana kwamba upelelezi unafanyika ili kujua ni nani ambaye ametenda kosa lile, bado suala la upelezi linaendelea, yapo maelekezo yaliyotolewa ambayo tunaendelea kufuatilia ili kuja kubaini, ikumbukwe silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndio ilikwenda ikamgusa Akwilina, lakini kama ulivyojua askari walikuwa ni wengi lakini pia kulikuwa hakuna ushahidi kwamba yupi aliyekuwa ametenda hivyo, kwa hiyo uchunguzi bado unaendelea”, amesema Kamnda Mambosasa.

Ikumbukwe kwamba mnamo Februari 17, mwaka huu, mwanafuzi wa chuo cha usafirishaji jijini Dar es salaam Akwilina Akwilini alifariki dunia baada ya kupigwa risasi ambayo inaaminika ilitoka kwa mmoja wa askari waliokuwa wakitawanya maandamano ya wafuasi wa chadema, huku yeye akiwa kwenye daladala akipita njia.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.