BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 9 February 2018

VIGOGO WATANO WA MADINI YA TANZANITE ONE WAKAMATWAMkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti aliagiza vigogo watano wachimbaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro na jijini Arusha, kukamatwa na polisi wakidaiwa kufadhili uchimbaji haramu wa madini hayo.


Leo Februari 8, 2018 kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara, Augostino Senga alisema vigogo hao walikamatwa jana jioni na kulazwa Kituo cha Polisi Mirerani.

Amesema wanawashikilia baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kupata taarifa kuwa, vigogo hao wanashiriki kuwadhamini vijana wanaoingia kwa wizi kwenye migodi ya kampuni ya TanzaniteOne yenye ubia wa asilimia 50 kwa 50 na Shirika la Madini la Taifa (Stamico).

Amesema wanachunguza suala hilo na iwapo vigogo hao ambao majina yao tunayo utakamilika, watafikishwa mahakamani


Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment