Type something and hit enter

By On

Daktari anamkagua mama aliyebeba mimba ya biashara katika kliniki ya Ilaya


Ukraine, ni miongoni mwa mataifa masikini barani Ulaya , na limeanza kuwa kivutio kikubwa kwa wanandoa wanaotaka kubebewa mimba .Fedha zinazopewa wanawake wanaoshiriki katika mpango huo zinawavutia wanawake wengi , lakini pia kuna changamoto zake.

Ana* alikuwa na miaka 18 wakati alipogundua kuhusu biashara ya kubeba mimba kupitia kwa runinga.

Alikuwa amemaliza shule ya upili na alikuwa na mpango wa kufanya kazi katika hoteli katika mji wa magharibi wa Ukrain ambapo watalii huzuru. Kazi hiyo hulipa $200 kwa mwezi , lakini kwa kumbebea mtu mwengine mimba aligundua anaweza kujipatia $20,000 (£14,000).

Familia ya Ana sio masikini kwa viwango vya kawaida. Mamake ni mhasibu na amekuwa akimsaidia kila mara.

Lakini anasema alivutiwa na biashara ya kubeba mimba , kwa kuwa alitaka kupata fedha ili kuweza kununua vitu vya ghali ,kurekebisha nyumba , gari na mambo mengine.

Ijapokuwa mamia ya wanawake hushiriki katika biashara hiyo ,mpango huo hauzungumziwi hadharani nchini Ukraine.

Wanandoa wa kigeni wamekuwa wakitembelea taifa hilo kwa wingi tangu 2015, wakati vituo vya kubeba mimba barani Asia vilipoanza kufunga viwanda vyao moja baada ya chengine , huku kukiwa na ripoti za unyanyasaji.

Huku wakizuiwa nchini India, Nepal na Thailand , waliamua kuelekea Ukraine ikiwa ni miongoni mwa maeneo machache ambayo yanaendelea na biashara hiyo pamoja na gharama kama ile ya Marekani.

''Tuna wanadoa wengi wasio na watoto wanaokuja katika taifa hili'', alisema Ana ambaye hakutaka kutambulishwa. Wakati alipokuwa na umri wa miaka 21 na baada ya miaka kadhaa ya kufanya kazi hotelini , Ana hatimaye alikubali kubeba mimba .

Wakati huo alikuwa na mtoto hatua iliomfanya kukubali.

Chini ya sheria ya Ukraine ,mama atakayebeba mimba lazima awe na mtoto wake mwenyewe kabla ya kushiriki katika biashara ya kubeba mimba ya mtu mwengine.

Iwapo una mtoto wako mwenyewe hautakuwa na mapenzi mengi na mtoto uliombeba , kulingana na wale wanaowaajiri wanawake hao.Ana anatumai atajinunulia jumba moja la ghorofa nyumbani kwao , Kamyanets-Podilskyi
Ni safari ndefu.

Ana alianza kuutazama mtandao ambao wanawake wanaobeba mimba za biashara , maajenti, kliniki na wafanyibiashara wa biashara hiyo huweka matangazo yao.

Na muda mfupi baadaye alielekea katika mji mkuu wa Kiev yapata kilomita 450 ili kukaguliwa kiafya.

Aliandikisha kandarasi na wanadoa kutoka Slovenia waliokuwa na tatizo la kupata mtoto.

Ana alikuwa na bahati, kiinitete kiliwekwa katika kizazi chake na kuanza mpango wote wa kubeba mimba kwa minajili ya biashara. Lakini ni wakati huo ambapo changamoto zilianza , anasema.

Anasema kuwa huduma za kiafya wanazopewa ni za kiwango cha chini, wanawake wengine waliobeba mimba walikuwa na matatizo ya kiafya ambayo hayakuangaziwa ama hata kutibiwa kwa wakati na hivyobasi kuzua matatizo mengine, anasema.

Aliweka malalamishi yake katika mtandao wa kijamii ili kuwaonya wanawake wengine lakini alikemewa na kliniki hiyo na sasa bado anaogopa kuwataja hadharani.

Mtoto aliyejifungua alizaliwa akiwa na afya njema lakini mpango wote ulikuwa wa kuogofya.

Bado, amekubali kwa mare nyengine kubeba mimba nyengine wakati huu akiwabebea wanadoa wa Japan. wanafuatilia maswala yote kupitia wakili mmoja mjini Kiev na kuna uwezekano mkubwa kwamba hatokutana nao ana kwa ana.

Ana wakati huu amekuwa na makini katika kuchagua kliniki ,lakini iwapo mpango wote utafanikiwa , kufikia miaka 24 atakuwa amejifungua watoto watatu , mmoja akiwa wake na wengine wawili wa mtu mwengine.IMama na watoto wake wawili wakitembea karibu na eneo la kumbukumbu la vita vya pili vya dunia katika eneo lililojaa theluji la Kamyanets-Podilskyi
Ukiwa mji mkuu wa Biashara ya kubeba mimba

Mahitaji ya kubeba mimba kwa lengo la kupata malipo nchini Ukraine yamepanda kwa asilimia 1000 katika kipindi cha miaka 2 iliopita pekee , anasema Sam Everringham wa shirika la familia kupitia ubebaji mimba wa biashara , shirika la hisani nchini Sidney ambalo huwashauri wanaotarajiwa kuwa wazazi.

Taifa hilo anaongezea, limejipata kwa bahati mbaya miongoni mwa mataifa ambayo yanaruhusu utalii wa kubeba mimba za biashara.

Licha ya kwamba sheria hiyo ni halali nchini Ukraine inawatambua wazazi wanaotarajiwa kuwa wazazi kutoka wakati mimba inaposhika na haitoi kiwango cha mwisho cha fedha ambazo anayebeba mimba hiyo atalipwa -hatua inayowapatia fursa wanaobeba kunadi bei.

Lakini haimaanishi kwamba ni swala la moja kwa moja. Ikitegemea unakotoka , mkakati wa kumtoa mtoto huyo nje ya taoifa hilo inaweza kuwa ndoto kali huku wanandoa kutoka mataifa kadhaa ikiwemo Uingereza wakilazimika kusalia nchini humo kwa miezi kadhaa.Image captionTangazo katika ukuta wa kliniki ya Ilaya linamuonyesha mama aliyebeba mtoto

Huku kliniki nyingi nchini Ukraine zikionekana kufanya kazi kwa uwazi na kuwahudumia wanawake hao vizuri washirika wengi katika sekta hiyo pamoja na wanawake wanaobeba mimba hizo huzungumzia kuhusu wale walio na sifa mbaya.

Kuna ripoti kadhaa ambazo hazijathibitishwa kuhusu viinitete vinavyobadilishwa na ukaguzi wa kiafya wa viwango vya chini

"Kuna mifano ambapo maajenti wa UKraine wamekataa kulipa gharama za kubeba mimba iwapo mbebaji atakiuka miko mikali , iwapo ataavya mimba'', kulingana na bi Everingham.

Kuna mifano mibaya ambapo maajenti hubadilika na kuwa wanyama iwapo mpango wa kubeba mimba haukuwafurahisha wazazi.Wanawake wanaobeba mimba za biashara wakisafiri kutoka Kiev kutoka nyumbani kwao kwa ukaguzi wa kila mara

Olga Bogomolets, daktari na mbunge ambaye anaongoza kamati ya bunge nchini Ukraine kuhusu afya anasema kuwa anaamini wanawake wadogo wanavutiwa na kubeba mimba za biashara kutokana na kuanguka kwa hali ya maisha katika taifa hilo.

Uchumi wa taifa hilo uliathiriwa na mfumuko mbaya 2014 na 2015 kutokana na mzozo unaoendelea mashariki mwa Ukraine kati ya jeshi na wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi.

Sekta hiyo kulingana na bi Bogomolets haijadhibitiwa vilivyo hivyobasi swala hilo linawaweka wabebabaji mimba na wazazi wanaolipa katika hatari

Wizara ya afya haijatoa tamko lolote kufuatia ombi la kutaka kufanya hivyo.Kuna orodha nyingi kama hii katika mitandao ya maajenti wa biashara ya kubaba mimbaTetiana akitembelea kliniki ya Ilaya

Tetiana anaishi na mamake lakini ameficha mimba alionayo akisema kuwa angependa kuelekea Kiev kutafuta kazi.Jana ambaye alijifungua mizezi miwli iliopita , anamshauri Tetiana anafaa kuchukulia biashara ya kubeba mimba kama kazi ya kawaida .

Anakumbuka mtoto aliyejifungua akichukuliwa mara tu alipojifungua huku akiwa amechoka katika kitanda chake.Anakiri kwamba hisia za kujifungua humjaa na alifikiria kuhusu mtoto huyo alipoelekea nyumbani.

Utakuwa mtu mbaya sana kutohisi hilo., anasema.lakini unapoona furaha na tabasamu kutoka kwa wazazi wenyewe, unagundua kwamba kila kitu kiko sawa na mtoto yuko katika hali nzuri.

Akiwa nyumbani na mwanawe magharibi mwa Ukraine, Ana pia anafikiria jukumu lake la kubeba mimba.Karibuni ataanza safari ya saa saba ya treni ili kuelekea kuelekea Kiev ili kuwekwa kiinitete katika kizazi chake.

Ijapokuwa ni hatua ngumu, ana matumaini ya kile atakachopata. Anataka kutumia fedha hizo kujinunulia jumba moja la ghorofa. Na pia anafurahia kile atakachowafanyia wazazi waliomlipa kuwabebea mimba.

''Wakati wanapobubujikwa na machozi ya furaha na kukushukuru, unahisi kitu ulichowafanyia'', anasema. Waliniambia kwamba mimi ni mtu muhimu sana katika maisha yao''.

Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment