RATIBA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CHADEMA KATA YA HANANASIF - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 19 February 2018

RATIBA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CHADEMA KATA YA HANANASIF


chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kinatarajia kuongoza shughuli za utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu wa chama hicho Kata ya Hananasif
Jimbo la Kinondoni, Daniely John siku ya kesho (Jumanne).


Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene jioni ya leo (Jumatatu) na kudai mwili wa marehemu Daniel unatarajiwa kufika nyumbani kwake Hananasif ukiwa unatokea hospitali ya Taifa Muhimbili majira ya saa 4 asubuhi na kisa kupelekwa katika Kanisa la Katoliki kwa ajili ya misa ya kumuombea marehemu itakayoanza saa 5 asubuhi kanisani hapo.

Baada ya ibada hiyo, waombolezaji watatoa heshima zao za mwisho kwa Daniel kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda mkoani Iringa ambako atazikwa siku ya Jumatano, katika kijiji cha Chikelewatu wilayani Mafinga.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ