BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 14 February 2018

RAIS JACOB ZUMA:SIONI SABABU YA KUJIUZULU


Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini amesema kuwa haoni sababu ya yeye kujiuzulu

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anasema hajafanya makosa na haoni sababu ya kujiuzulu.

Bwana Zuma alizungumza baada ya chama tawala cha ANC kumpatia makataa ya kujiuzulu mwisho wa siku la sivyo akabiliwe na kura isiokuwa na imani dhidi yake siku ya Alhamisi.

Rais huyo amekuwa chini ya shinikizo ya kujiuzulu huku kukiwa na madai mengi ya ufisadi.

Lakini amesema kuwa ANC imeshindwa kuelezea ni kwa nini ametakiwa kujiuzulu.

''Haijakuwa haki kwangu mimi kwamba tatizo hili limeangaziwa'', aliambia kituo cha habari cha SABC wakati wa mahojiano marefu ambayo hayakuwa yametangazwa rasmi.

''Hakuna mtu aliyetoa sababu .Hakuna mtu anayesema kilichofanyika'', Alisisitiza kwamba hakipuuzi chama cha ANC lakini amekataa kukubaliana na uamuzi wa kumtaka kujiuzulu.

Bwana Zuma amesema kuwa yuko tayari kuondoka baada ya mwezi Juni , lakini akapinga vile jambo hilo linavyoangaziwa kwa sasa .Alisema kwamba atatoa taarifa nyengine baadaye siku ya Jumatano.

Chama cha ANC kimesema kuwa kilisikiza matamshi ya Bwana Zuma lakini kitatoa uamuzi wa hatua yake baadaye kabla ya kuzungumza.

Awali kiranja wa chama hicho Jackson Mthembu alitangaza kwamba kura isiokuwa na imani dhidi ya rais itasikizwa siku ya Alhamisi huku Cyril Ramaphosa aliyechaguliwa kuwa rais wa chama hicho mwezi Disemba akiapishwa mara moja kuwa rais wa taifa hilo.

Mkutano wa kamati kuu ya ANC ulikuwa umetangaza uamuzi wake wa kumtaka Zuma ajiuzulu siku ya Jumanne na kumpatia hadi mwisho wa siku siku ya Jumatano kujiuzulu.Familia ya Gupta imetuhumiwa kwa kutumia uhusiano wa karibu na rais kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa.SOUTH AFRICAN PRESIDENCYImage captionAtul Gupta akisalimiana na rais Zuma

Katika mahojiano , bwana Zuma hakuzungumza kuhusu uvamizi wa mapema alfajiri uliotekelezwa na maafisa wa polisi katika nyumba ya washirika wake wakuu familia ya Gupta siku ya Jumatano.

Familia ya Gupta imetuhumiwa kwa kutumia uhusiano wa karibu na rais kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa.

Pande zote mbili zimekataa kuwepo kwa madai hayo.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment