OMBI LA JPM KWA WATANZANIA AKIWA IBADANI WILAYANI CHATO - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 25 February 2018

OMBI LA JPM KWA WATANZANIA AKIWA IBADANI WILAYANI CHATORais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wananchi wa mkoa wa Mwanza waendelee kumuombea katika sala zao wanazozifanya kwa kuwa kazi yake ni kubwa mno na inahitaji maombi ya hali ya juu.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati aliposhiriki ibada ya Dominika ya pili ya Kwaresma - Parokia ya Chato Mkoani Mwanza leo (Jumapili) baada ya kupewa shukrani na Padri Alex Elias Bulandi (Msaidizi Parokea ya Chato) kwa msaada alioutoa wa kukamilisha ujenzi wa nyumba ya ibada ili waweze kujumuika waumini wengi katika kanisa hilo.

"Nazidi kusisitiza maneno mazuri aliyeyazungumza Padri kwamba tunawajibu wa kujiweka tayari katika maisha yetu kwa sababu maisha yetu ni ya kupita, tupendane siku zote tuendelee kumtanguliza Mungu na mimi nahitaji sana sala zenu, kazi hii ni ngumu inahitaji maombi na ndio maana nawaomba ndugu zangu muendelee kumtanguliza Mwenyezi Mungu katika sala kwa mambo yote ili kusudi tuweze kutimiza wajibu wetu kama mapenzi ya Mwenyezi Mungu yanavyotaka", amesema Dkt. Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Magufuli jana (Jumamosi) wakati akiwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea Mjini Kampala, Uganda kwenye mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amewaahidi wananchi wa mkoa huo kuwa serikali itafanyia kazi mahitaji ya kujengwa kwa jengo la abiria pamoja na ujenzi wa uzio ili uwanja wa Mwanza uwe na hadhi ya kimataifa na hivyo kuiwezesha nchi kupata mapato zaidi.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ


Subscribe to EDUSPORTSTZ